Sunday, October 9, 2011

Poulsen ataja First XI

Taifa Stars
Kocha Jan Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 11 ambao wataanza kwenye mechi ya leo dhidi ya Morocco. Mechi hiyo inaanza saa 1.30 usiku kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania ni saa 4.30 usiku na itachezwa Grand Stadium hapa Marrakech. Poulsen atatumia mfumo wa 4-4-1-1 huku akimweka Mbwana Samata kuwa mshambuliaji wa mwisho na nyuma yake akicheza Abdi Kassim.
Katika kikosi cha kwanza amewaanzisha wachezaji wote wa kulipwa wanaocheza nje ya Tanzania ambao anao hapa. Amewataka wachezaji kuwa focussed na mchezo, kujituma na kila mmoja kutekeleza wajibu wake uwanjani ili ushindi uweze kupatikana. Baada ya kutoa game plan yake, Poulsen aliwaonesha wachezaji CD ya mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Morocco ambapo tulifungwa bao 1-0.
Kupitia CD hiyo aliwaeleza wachezaji upungufu uliojitokeza na pia wachezaji hatari wa Morocco wanaotakiwa kuangaliwa kutokana na uzuri wao wanapokuwa uwanjani. Amewakumbusha mabeki kuwa mshambuliaji Chamakh Marouane (Arsenal, Uingereza) kuwa ni mzuri kwa mipira ya vichwa, hivyo kutomuacha kuruka peke yake katika mipira hiyo.
Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Idrisa Rajab, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Shabani Nditi, Mohamed Rajab, Henry Joseph (Captain), Mbwana Samata, Abdi Kassim na Dan Mrwanda.

Subs: Shabani Dihile, Nassoro Cholo, John Bocco, Ramadhan Chombo, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Jabir Aziz

Iniesta nje Mwezi Mmoja


 
 
Klabu ya Barcelona imetangaza kwenye mtandao wake kwamba, Andres Iniesta atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja.

Kiungo huyo aliumia dakika 5 kabla ya mapumziko, kwenye mechi ambayo timu yake ilitoka sare ya 2-2 na AC Milan, katika michuano ya Kombe la mabingwa Barani Ulaya siku ya Jumanne.

Iniesta atakosa mechi dhidi ya Osasuna, Valencia, Atletico Madrid, BATE Borisov na Sporting Gijon.

Mchezaji huyo anategemea kurudi tena uwanjani kwenye mechi ya michuano ya Euro 2012, ambapo timu ya Hispania itakapocheza na Czech Republic na Scotland, mnamo tarehe 7 na 11 Oktoba.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ameweza kucheza jumla ya mechi 6 kwa klabu msimu huu, huku akikamilisha wastani wa dakika 469 uwanjani.

Bradley aajiriwa Misri

 
 
Inaarifiwa kwamba, Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Marekani Bob Bradley, ameajiliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Misri.

Msemaji wa EFA Azmy Megahed amesema, Bradley anategemea kuwasili Cairo wikiendi hii kukamilisha mpango huo.

"Kila kitu kipo sawa. Bradley atawasili hapa siku ya Jumapili kukamilisha mkataba," Megahed alisema.

Bradley atakuwa amechukua nafasi ya kocha wa kipindi kirefu wa timu hiyo Hassan Shehata, ambaye kibarua chake kilisitishwa mnamo mwezi June, kufuatia kufanya vibaya kwa timu hiyo kwenye kampeni zake za kushiki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2012.

Timu hiyo mpaka sasa imetolewa kwenye mbio hizo.

Bradley aliiwezesha Marekani kufika kwenye mzunguko wa 16 wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, iliyofanyika nchini Afrika ya Kusini.

Na alipigwa chini mnamo mwezi July baada ya Marekani kufungwa 4-2 na Mexico kwenye fainali ya Gold Cup, huku nafasi yake ikichukuliwa na kocha wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann.

Bradley atakuwa na mtihani mzito kuhakikisha nchi ya Misri inapata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia, kwa mara ya mwisho Taifa hilo kushiriki Kombe hilo ilikuwa ni mwaka 1990.
.
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Polisi Dodoma iliyochezwa Septemba 14 mwaka huu Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 16,839,000.

Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 2,257 ambapo kiingilio kilikuwa sh, 7,000 kwa mzunguko na sh. 20,000 kwa VIP. Waliokata tiketi za sh. 20,000 walikuwa 80.

Baada ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 2,568,661.02 kila timu ilipata sh. 3,546,671.90. Mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 1,162,893.90), TFF (sh. 1,162,893.90), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 581,446.95), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 465,157.56) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 116,289.39).
Wayne Rooney
 
Meneja wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson, amemfananisha mshambuliaji wa timu yake Wayne Rooney na mchezaji mkongwe wa Brazil Pele.

Fergie ameyasema hayo, kuelelekea kwenye mechi ya Kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya dhidi ya Benfica, mechi inayotarajiwa kuchezwa usiku huu, huku mchezaji huyo akionekana kuwa kwenye kiwango kizuri kiuchezaji.

Upatikanaji wa Tiketi mechi za Simba na Yanga Uwanja wa Chamazi

Tiketi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zinazohusisha timu za Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam hazitauzwa uwanjani. Lengo ni kuwaondolea usumbufu mashabiki ambao wanakwenda kwenye mechi hizo na kukuta tiketi zimekwisha, hivyo kuweza kuwa chanzo cha vurugu.

Ili kujiridhisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilifanya uhakiki na kubaini Uwanja wa Azam una uwezo wa kuchukua watazamaji 5,000 tu na si 7,000 kama ilivyoelezwa awali. Hata hivyo lengo la mmiliki wa uwanja huo ni kuongeza viti hadi kufikia 7,500.

Kwa mantiki hiyo tiketi zitakazouzwa kwa mechi za Yanga na Simba kwenye uwanja huo ni 5,000 tu. Vituo vya kuuzia tiketi hizo siku moja kabla ya mchezo na siku yenyewe ya mchezo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kituo cha Mafuta cha OilCom kilichoko Ubungo na Mbagala Rangitatu.

Viingilio kwa mechi za timu hizo zitakazochezwa Uwanja wa Azam ni sh. 20,000 kwa jukwaa kuu lenye uwezo wa kuchukua watazamaji 400 wakati majukwaa ya kawaida itakuwa sh. 7,000. Ili kuhakikisha idadi ya mashabiki haizidi uwezo wa uwanja hakutakuwa na tiketi za bure (complimentary).

Hivyo kutokana na kuwepo vituo vya kuuzia tiketi katika maeneo yaliyotajwa, mashabiki ambao watakosa tiketi hawana sababu ya kwenda uwanjani. Simba na Yanga zitaanza kuutumia uwanja huo kesho (Septemba 14 mwaka huu) kwa Simba kuwa mwenyeji wa Polisi Dodoma wakati siku inayofuata Yanga itakuwa mgeni wa African Lyon.

Sendeu kwa Pilato Tibaigana

Luis Sendeu
 
Sekretarieti ya TFF itawasilisha mashtaka dhidi ya Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu kwenye Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi inayoongozwa na Kamishna wa Polisi mstaafu Alfred Tibaigana kutokana na matamshi yake dhidi ya mwamuzi Alex Mahagi.

Mara baada ya mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyochezwa Septemba 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, Sendeu aliita mkutano na waandishi wa habari na kumshutumu Mahagi kuwa alisababisha timu yake ikose ushindi kwa kuwabeba wapinzani wao.

Aliongeza kuwa anamfahamu Mahagi kuwa ni mwanachama wa Simba, kadi nyekundu aliyompa kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima si halali na alifanya hivyo kwa lengo la kuisadia Simba ili iendelee kukaa kileleni mwa ligi.

Kauli ya Sendeu ililenga kumjengea chuki Mahagi mbele ya mashabiki wa Yanga kama ilivyo kwa viongozi na watendaji wa TFF. Ni wazi Sendeu akiwa ofisa wa Yanga anajua taratibu za kufanya pale klabu yake isiporidhishwa na uamuzi wa mwamuzi au suala lingine lolote.

Matamshi ya Sendeu yanalenga kuchochea chuki na vurugu katika mpira wa miguu ambapo ni kinyume na Ibara ya 53(1) na (2) ya Kanuni za Nidhamu za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Monday, September 5, 2011

Santos: Hakuna makubaliano ya kuuzwa Neymer

Neymar

Klabu ya Santos  ya nchini Brazil imesema haijafikia makubaliano na timu yoyote juu ya uwezekano wa kumuuza mshambuliaji wake Neymar.

Klabu hiyo imetoa tamko hilo Jumapili kwenye taarifa ndefu waliyoitoa kwenye Mtandao wake, taarifa hiyo imesisitiza kwamba, hakuna dili yoyote ambayo wamefikia na Barcelona juu ya kumuhamisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, kwenda Camp Nou ifikapo mwaka 2013.

"Kutokana na sababu binafsi zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni kuhusiana na Neymar, Santos Futebol Clube inapenda kutoa tamko rasmi kwamba, maelezo yanayotolewa na vyombo hivyo juu ya mustakabali wa Neymer sio za kweli” taarifa hiyo ilisema.

"Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu mara zote imekuwa na nia njema ya kuendelea kubaki na Neymer kwenye timu.”

Taarifa hiyo imekuja baada ya gazeti la Estadao siku ya Jumamosi kuandika kwamba, Santos na Barcelona wamefikia makubaliano ya awali kwa Neymar kujiunga na mabingwa Hispania na Ulaya baada ya miaka miwili toka sasa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Bazil amekuwa akihusishwa na kuhamia Barcelona na pia kwa mahasimu wao Real Madrid katika kipindi cha majira ya joto, huku baadhi ya timu nyingine za Bara la Ulaya zikihusishwa juu ya mpango huo, ila mchezaji juyo amekuwa akisisitiza kwamba kwa muda huu angependa kuendelea kucheza nchini mwake.

Del Piero: Bado sijaamua mwisho wangu

Alessandro Del Piero

Mchezaji mkongwe wa Juventus Alessandro Del Piero, amesema bado hajaamua kama ataendelea kucheza mpira baada ya msimu huu wa 2011-12.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, bado yupo kwenye mkataba unaomuweka mpaka mwezi June mwakani pale Turin, ila inaelezwa kwamba mwisho wa mkataba huo haimaanishi kwamba na yeye atastaafu.

"Kufikiria juu ya mwisho wangu kwenye soka , si kitu ambacho kinanichukulia muda kuamua. Bado sijaamua kama huu utakuwa ni mwisho wangu kucheza na Juventus," Del Piero alieleza La Gazzetta dello Sport.

"Kufikiria juu ya kwamba huu ni mwaka wangu wa mwisho inanifanya nijitoe kwa zaidi ya asilimia 200. Nahitaji kumaliza kipindi changu kwenye mafanikio ya juu.  Nikijaribu kuangalia nyuma miaka 20 iliyopita, nitaangalia nikiwa nimeridhika sana."

Del Piero alianza kucheza kwenye kiwango cha juu akiwa Padova, ila akajiunga na Juventus mnamo mwaka 1993. Mchezaji huyo mpaka sasa ameweza kucheza jumla ya mechi 600 kwa timu hiyo ya Serie A.

Capello: Barcelona Watafungika

Fabio Capello

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amesema kwamba, anaamini haitachukua muda kwa timu ntingine kupata jibu juu ya aina ya mpira ambao timu ya Barcelona inaucheza.

Timu hiyo ya Catalans inaaminika na watu wengi kwamba ni timu kali ambayo haijawahi  tokea duniani, ila Capello anaamini kwamba utawala wao hautakuwa wa milele.

"Naweza kumuona mtu anayeweza kuizuia Barcelona kwa siku za mbele? Nafikiri ndio. Itawezekana, sababu tuna bahati kwamba tunaweza kuwasoma wapinzani," Capello alinikuliwa kwenye mtandao wa FIFA.
"Utapata ufumbuzi wa namna ya kuizuia Barcelona, kwa kuelewa uwezo wao. Utajifunza mengi, ukiangalia mchezo wao kwenye mikanda. Naamini baadhi ya timu zitapata dawa ya kuifunga."

Pia anaamini kwamba taratibu kama ilivyo asili ya mchezo kiwango chao kinaweza kushuka.

Akaendelea kusema "Unapokuwa unashinda mara nyingi, wakati mwengine  unakuwa unakosa kitu kinachokufanya uwe makini kwa kila mchezo kuweza kushinda, wachezaji wengine pia wanazeeka kimchezo."

Barcelona wameshinda Kombe la Mabingwa Ulaya msimu uliopita, na wameanza msimu mpya wa 2011-12, wakiwafunga wapinzani wao Real Madrid kwenye Supercup ya nchini kwao Hispania, halafu wakaja kuwafunga Porto kwenye Supercup ya Ulaya.

Mchezaji Bora wa Wiki Goal.com

Cesc Fabregas

Cesc Fabregas Mchezaji Bora wa Wiki Goal.com
Klabu: Barcelona

Nchi:Hispania

Miaka: 24
Nafasi: Kiungo

Mafanikio: Amesaidia ushindi kwa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania

Terry: Don't write off Lampard


England captain John Terry has voiced his full support for dropped midfielder Frank Lampard.

An injury-free Lampard was left out of a competitive England starting XI for the first time since 2007 with a midfield trio of Scott Parker, Gareth Barry and Ashley Young preferred for the 3-0 Euro 2012 qualifier win over Bulgaria last Friday.

There have been suggestions that Lampard's exclusion could be the beginning of the end of the 33-year-old's international career, but his Chelsea team-mate Terry has issued a warning to the doubters.

Speaking ahead of Tuesday's meeting with Wales at Wembley, Terry said: "Write Frank Lampard off at your peril. I have known him an awful long time and he was disappointed about not starting but trained incredibly hard the day after and he remains one of the best players I have ever played with.

"Because of his age people tend to write him off but he is still in excellent form. His record for England has been incredible.''

Twiga Stars yalala dhidi ya Ghana

 
 
Timu ya wanawake ya Taifa ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza mechi yake ya kwanza ya michezo ya All Africa Games (AAG) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Ghana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machava, jijini Maputo.
 
Kwa mujibu wa Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis hadi mapumziko timu hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Mwanahamisi Shuruwa aliisawazishia Twiga Stars dakika ya 85, lakini Ghana ikapata bao la pili dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.
 
Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili Septemba 8 mwaka huu dhidi Afrika Kusini. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi itakuwa Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.

TFF yatangaza mapato ya pambano la Stars

Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) limeingiza sh.148,220,000. Mechi hiyo ilichezwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,892. Viti vya kijani ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo 17,650 ikiwa ni zaidi ya nusu ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo.

VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 30,000, jumla ya mashabiki 394 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. Viti vya bluu ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa ni 8,166.

Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 7,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 VIP C na sh. 20,000 VIP B

Sunday, September 4, 2011

TFF yachakachua Ratiba Ligi Kuu

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana lilitangaza tena kuipangua ratiba ya mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo inaendelea nchini katika viwanja mbalimbali.

Akizungumza jana, Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa mechi namba 19 kati ya Simba na Villa Squad (zote za Dar es Salaam), iliyopangwa kufanyika Septemba 8, sasa itachezwa Septemba 7 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Wambura alisema vilevile kuwa mechi kati ya Azam na Simba, sasa itachezwa Septemba 10 kwenye Uwanja wa Mkwakwani na hilo limetokana na nia ya kuipa unafuu Azam ambayo itakuwa ikitokea Arusha kucheza dhidi ya JKT Oljoro na kupata fursa ya kumaliza mechi zao kwenye kanda hiyo.

Wambura pia alisema kuwa Kamati ya Mashindano ya TFF imeisogeza mbele kwa siku moja mechi kati ya Coastal Union ya Tanga dhidi ya Moro United ya Dar es Salaam ambapo sasa itachezwa Septemba 8.

Imebainika kuwa ratiba ya awali iliyotolewa na kamati hiyo itakayomalizika Aprili Mosi mwakani itaendelea kupanguliwa kila mara kwani bado haijatoa nafasi kwa timu za Yanga na Simba ambazo mapema mwakani zitashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Morocco 0 Central African 0



Morocco and Central African Republic stay level on points at the top of Group D, after a 0-0 draw - a result that will be of far more value to the Moroccans, on what could have been tricky trip to Bangui.
The Atlas Lions had plenty of chances in the first half and had a goal disallowed, but the home side managed to keep them at bay and exert their own share of pressure, with both sides drawing a blank in their penultimate qualifying fixture.
The result leaves the group poised for final day drama, with Tanzania and Algeria also still in with contention, after drawing 1-1 on Saturday.
________________________________________________________

Uganda will have to wait until their final Africa Cup of Nations qualifier against neighbours Kenya next month after falling to a 2-0 defeat in Angola.
The result - Uganda's first defeat of the campaign - keeps them at the top of their group, but only by a point from Angola, as the east Africans seek to secure their first appearance at the Nations Cup since 1978.
Elsewhere, Niger leapt to the top of Group G, with a 2-1 victory over South Africa, while Nigeria's vital 2-0 away win in Madagascar was overshadowed by Guinea's 1-0 defeat of Ethiopia, which keeps them three points clear of the Super Eagles.
The BBC's Stephen Fottrell rounds up all the details of the day's action below.
_________________________________________________________
In Group A, Zimbabwe beat Liberia 3-0 in Harare to go second in Group A behind Mali, who defeated Cape Verde 3-0 on Saturday.
Goals from Wilard Katsande, Ovidy Karuru and Khama Billiat secured a convincing victory for the Warriors.
The result takes the group down to the wire on the last day, with Mali away to Liberia and Zimbabwe away to Cape Verde next month.
_________________________________________________________
In Group B, two second-half goals gave Nigeria a valuable 2-0 away win in Madagascar.
The Super Eagles overcame poor playing conditions to claim victory in the last 20 minutes, with goals from skipper Joseph Yobo and a long-range effort from Obinna Nsofor sealing a much-needed win.
The result puts them second in the group behind Guinea, who beat Ethiopia 1-0 to remain top of the table.
Nigeria will now have to beat Guinea by at least two goals on the final day to top the group on the head-to-head rule.
_________________________________________________________
In Group C, Zambia earned a 2-1 victory away to Comoros to put them top of the group and line up a winner-takes-all showdown in Lusaka against Libya in the final round of qualifiers.
The Chipolopolo left it late to take all three points in Moroni, hitting a late winner, having earlier taken the lead through a Christopher Katongo goal, before seeing the Comoros equalise.
Libya beat Mozambique 1-0 on Saturday, in a match played in Cairo because of the civil unrest in Libya, to set up a tight finale to the group.
________________________________________________________
In Group G, Niger secured a massive home victory over South Africa, beating Bafana Bafana 2-1 in Niamey, to put them top of the table.
Dankwa Kofi put the home side ahead in the first half, heading home from a corner, before Mazour doubled their lead from close range.
South Africa pulled one back through Jali but Niger held on for a win that puts them closer to a coveted appearance at the 2012 finals.
With champions Egypt out of contention after losing 2-1 to Sierra Leone on Saturday, the group comes down to a three-way shoot-out for top spot on the final day between Niger, South Africa and the Leone Stars.
________________________________________________________
Burundi grabbed a late equaliser against Benin to share the points in Bujumbura and keep the two teams level on points in Group H.
Papy Faty scored the equaliser for Burundi in the 90th minute, after Guy Akpagba's opener for Benin on 55 minutes.
The result keeps the teams in joint second place in the group, behind Ivory Coast who had already qualified before thumping Rwanda 5-0 on Saturday.
________________________________________________________
Sudan secured a highly valuable 1-0 away win in Congo Brazzaville to bring Group I down to the wire next month.
The result, secured thanks to a second-half goal from Bakri Abdelgadir, puts the Sudanese level on 13 points with Ghana at the top of the group.
The Black Stars beat Swaziland 2-0 on Saturday but will have to wait until October for a winner-takes-all showdown with their fellow group leaders.
________________________________________________________
Uganda began the day in a position to secure their first Nations Cup finals berth in more than 30 years, but will have to wait until their final qualifier against Kenya, after falling to a 2-0 defeat in Angola.
The result - Uganda's first defeat of the campaign - keeps the Cranes top of Group J, but only by a point from Angola.
Kenya are also still in contention, after beating Guinea Bissau 2-1 on Saturday, as the group heads for a fascinating final day climax.
________________________________________________________
Togo earned their first win of the campaign against runaway Group K winners Botswana.
Their 1-0 win, however, matters little as they have no chance of qualifying, whereas Botswana booked their ticket to the finals long before what was their final game of the group.
Malawi still retain the edge in the race towards the automatic second-place qualification spot in the group, after their 0-0 draw with Tunisia on Saturday - a result which leaves them both tied on points, but gives Malawi a superior head-to-head record.

Capello: Lampard inabidi ajipange

Frank Lampard

Kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza Mtaliano Fabio Capello, amemuonya Frank Lampard na nyota wote wakongwe wa Uingereza kwamba, wasiwe na uhakika wa namba kwenye kikosi cha wachezaji XI wa kwanza.

Lampard, 33, ambaye ameshacheza jumla ya mechi 87 za Uingereza, aliachwa kwenye benchi mpaka dakika ya 80 alipoingia, wakati Uingereza ikiwa mbele kwa 3-0 dhidi ya Bulgaria, ambapo Capello aliamua kuwaanzisha Scott Parker na Gareth Barry kwenye kiungo cha kati.

Meireles akana Pesa kumuondoa Liverpool

Raul Meireles

Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Raul Meireles, amesisitiza kwamba hela si kitu ambacho kilimshawishi kufanya uhamisho wa kushtukiza toka Liverpool na kuhamia Chelsea.

"Haya ni mambo yanayotokea kwenye mpira wa miguu. Nitasema vitu vizuri tu kuhusu Liverpool, nilikuwa na mwaka mmoja mzuri," Meireles aliieleza RTPN.

"Watu wanafikiri mimi ni Yuda na nilihama kwa sababu ya hela. Hiyo haikuwa sababu, nitaelezea wakati mwengine, kwa sasa bado ni mapema.

"Ilitokea haraka sana, mimi si mtu wakulaumiwa kwa kitendo changu cha kuondoka Liverpool, ila sitaacha kuipenda Klabu sababu nina marafiki wazuri sana pale.

"Kitu cha msingi ni kutumia muda wangu wote kuitumikia Chelsea iweze kushinda mataji." Alisema Meireles.

Meireles anategemea kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Chelsea mnamo September 10, wakati timu hiyo inayojulikana maarufu kama The Blues watakapocheza na Sunderland.

Sneijder: Mourinho aliniambia nibaki Inter

Wesley Sneijder

Nyota wa Klabu ya Inter Milan Wesley Sneijder, amefunguka tena na safari hii akisema Kocha wake wa zamani Jose Mourinho, alimwambia awatose Manchester United na aendelee kubaki San Siro.

"Mourinho alinipigia simu akaniambia hivyo. Jamaa ana moyo na timu ya Inter na mara zote amekuwa akinieleza nibaki," Sneijder alilieleza La Gazzetta dello Sport.

"Niko na furaha kwa kubaki hapa, sikuwahi kutaka kuondoka na sitaki kuendelea kuzungumzia kuhusu Manchester United."

"Wakala wangu aliniambia Inter wanataka kuniuza. Tayari nimeongea na Manchester United. Mara ishu juu ya kuuzwa kwa Eto'o ikaanza, hapo mambo yakabadilika," alielezea mchezaji huyo wa kimataifa toka Uholanzi.

Licha ya maelezo yake Sneijder kwamba yuko na furaha hapo Inter, vyombo vya habari nchini Uingereza vimekuwa na taarifa nyingi tofauti vikieleza juu ya uhamisho huu, zaidi ni juu ya uwezekano wa uhamisho huu kufanyika mwezi wa January.

Barcelona: Fabregas Ana Thamani ya £53m

Cesc Fabregas  

Makamu wa Rais wa Klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu, anaamini kwamba Cesc Fabregas ana thamani ya £53ml, hela ambayo klabu yake ya awali Arsenal ilikuwa inahitaji kuweza kumuuza mchezaji huyo kwa Barca.

Makamu wa Rais huyo amesema, katika kipindi kifupi alichomuona akiitumikia Barcelona na Hispania kwa ujumla, amemkubali sana.

"Baada ya kuona kazi anayoifanya toka awasili hapa, hakika Cesc thamani yake inafika €60ml sawa na £53ml ambazo Arsenal walizihitaji," alisema Bartomeu. "Kijana anacheza kwa kiwango cha juu, na katika kipindi cha wiki tatu ya mazoezi uwezo wake ni wakushangaza . Hakika uhamisho huu ni mzuri, kimasoko hii iko wazi, si yakuficha Cesc ana thamani ya hela nyingi sana.