Sunday, September 4, 2011

Meireles akana Pesa kumuondoa Liverpool

Raul Meireles

Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Raul Meireles, amesisitiza kwamba hela si kitu ambacho kilimshawishi kufanya uhamisho wa kushtukiza toka Liverpool na kuhamia Chelsea.

"Haya ni mambo yanayotokea kwenye mpira wa miguu. Nitasema vitu vizuri tu kuhusu Liverpool, nilikuwa na mwaka mmoja mzuri," Meireles aliieleza RTPN.

"Watu wanafikiri mimi ni Yuda na nilihama kwa sababu ya hela. Hiyo haikuwa sababu, nitaelezea wakati mwengine, kwa sasa bado ni mapema.

"Ilitokea haraka sana, mimi si mtu wakulaumiwa kwa kitendo changu cha kuondoka Liverpool, ila sitaacha kuipenda Klabu sababu nina marafiki wazuri sana pale.

"Kitu cha msingi ni kutumia muda wangu wote kuitumikia Chelsea iweze kushinda mataji." Alisema Meireles.

Meireles anategemea kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Chelsea mnamo September 10, wakati timu hiyo inayojulikana maarufu kama The Blues watakapocheza na Sunderland.

No comments:

Post a Comment