Friday, September 2, 2011

Milan Wamtema Inzaghi Kwenye Kikosi Cha Ligi Ya Mabingwa Ulaya


Filippo Inzaghi

Mshambuliaji mkongwe wa timu ya AC Milan Filippo Inzaghi, ametemwa kwenye kikosi cha AC Milan kitakachoshiriki kwenye Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya msimu huu, hii inamfanya Inzaghi ashindwe kuvunja rekodi ya ufungaji wa mabao inayoshikiliwa na Raul kwa sasa.

Akiwa amecheza mechi 115 na kufunga magoli 70, Inzaghi anaendelea kuwa nyuma ya Raul ambaye mpaka sasa amemtangulia kwa magoli mawili zaidi, Raul ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wanaoheshimika na Real Madrid, ana jumla ya magoli 72 katika michuano hiyo.

Na kwa umri wa miaka 38 alionao Inzaghi, inaonyesha moja kwa moja mchezaji huyo tamati yake ndio imefika, na itakuwa ngumu kuweza kulinyakua tena taji ambalo Raul alilipora kwake msimu uliopita.

Msimu uliopita kwenye ligi hiyo Raul alifunga magoli matano akiwa na timu ya Schalke ya nchini Ujerumani, na kuweza kumpiku gwiji huyo aliyekuwa anaongoza kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment