Thursday, September 1, 2011

Sneijder: Najisikia Furaha Kubaki Inter

Wesley Sneijder kwenye Mahojiano na AD

Mchezaji wa Inter Milan Wesley Sneijder ameebainisha kwamba alikuwa karibu kujiunga na Manchester United, ila akasisitiza anajisikia furaha kubaki Inter.

Sneijder amehusishwa na mpango wa kuhamia Old Trafford katika kipindi chote cha majira ya joto.

"Nilihisi uhamisho wangu kwenda Man U uko karibu," Sneijder aliieleza AD. "kulikuwa na mazungumzo kwa mara kadhaa. Ukweli ni kwamba Inter ilikuwa inahitaji kuuza wachezaji, ilikuwa awe Eto'o au mimi. Nia ilikuwepo, ila kutokana na mkanganyiko wa mambo haikuwezekana"

Akaendelea kwa kuongeza "Wao ni moja kati ya klabu kubwa Duniani, kwa hiyo haikuwa mbaya kwangu kujiunga nao, ila kwa kipindi hicho hicho sikuwa nataka kuondoka Inter. Nipo Italia na na kwangu hicho ni kitu kikubwa sana"

Moja kati ya sababu zilizofanya mpango huu kutokamilika ni ishu ya mshahara wa mchezaji huyo kuwa mkubwa, na juu ya hilo Sneijder akasema "Kwangu mimi haikuwa hasa ni ishu ya mkwanja, hapa Inter mambo ni mazuri, naipenda hii Klabu, watu wa Italia na utamaduni wao unaendana na mimi"

No comments:

Post a Comment