Sunday, September 4, 2011

Sneijder: Mourinho aliniambia nibaki Inter

Wesley Sneijder

Nyota wa Klabu ya Inter Milan Wesley Sneijder, amefunguka tena na safari hii akisema Kocha wake wa zamani Jose Mourinho, alimwambia awatose Manchester United na aendelee kubaki San Siro.

"Mourinho alinipigia simu akaniambia hivyo. Jamaa ana moyo na timu ya Inter na mara zote amekuwa akinieleza nibaki," Sneijder alilieleza La Gazzetta dello Sport.

"Niko na furaha kwa kubaki hapa, sikuwahi kutaka kuondoka na sitaki kuendelea kuzungumzia kuhusu Manchester United."

"Wakala wangu aliniambia Inter wanataka kuniuza. Tayari nimeongea na Manchester United. Mara ishu juu ya kuuzwa kwa Eto'o ikaanza, hapo mambo yakabadilika," alielezea mchezaji huyo wa kimataifa toka Uholanzi.

Licha ya maelezo yake Sneijder kwamba yuko na furaha hapo Inter, vyombo vya habari nchini Uingereza vimekuwa na taarifa nyingi tofauti vikieleza juu ya uhamisho huu, zaidi ni juu ya uwezekano wa uhamisho huu kufanyika mwezi wa January.

No comments:

Post a Comment