Alvaro Pereira
Alvaro Pereira amesisitiza kwamba anaheshimu maamuzi ya timu yake ya Porto ya kukataa ofa ya Klabu ya Chelsea ya kutaka kumsajili yeye.
Chelsea walijaribu mpaka siku ya mwisho kumnasa winga huyo toka Uruguay ikashindikana, mchezaji huyo pia anaweza kucheza nafasi ya kiungo.
Porto walikuwa wanahitaji kiasi cha £25m toka kwa kocha wa zamani wa timu hiyo Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ni kocha wa Chelsea, ili aweze kuungana tena na mchezaji huyo pande za Stamford Bridge.
Dau hilo likaonekana kubwa na Chelsea wakashindwa kufikia matakwa ya Porto, hivyo kumfanya Pereira aendelee kubaki na mabigwa hao wa Europa League.
"Klabu ilikataa hiyo ofa, nami nitaendelea kuwa kwenye rangi za Porto” Pereira aliieleza Sport 890 ya Uruguay.
"Walisema hawakutaka kuniuza na kuidhohofisha timu, na mimi kama mchezaji sina budi kuheshimu maamuzi.
"Chelsea walichoshwa na hiyo hali ikabidi wajitoe. Wakala wangu alinieleza kwamba timu hizi mbili zimeshindwa kufikia makubalianao.
"Nahitaji kujikita zaidi na Porto kwa sasa huku nikijaribu kuwa na mcheza mzuri, itakuwa sio rahisi ila hiyo ni changamoto kwangu." Alisema Pereira.
Ilielezwa kwamba Chelsea walikuwa wapo tayari kutoa ofa ya €20m, wakianza kwanza kutoa €10m kwa mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment