Nizar Khalfan
Wachezaji Nyota wa Tanzania wanaokipiga nje ya nchi wamewataka mashabiki na wadau wote wa soka kujitokeza kwa wingi kesho kwenye Uwanja wa Taifa na kuwapa sapoti ya kutosha kwani wamekuja kivingine na kuahidi ushindi mkubwa dhidi ya Algeria.
Nyota hao saba ni Nizar Khalfan (Vancouver WhiteCaps, Canada), Danny Mrwanda na Abdi Kassim (Don Long, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Henry Joseph, Athuman Machupa na Idrissa Rajabu (Sofapaka, Kenya).
Pambano hilo la kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika nchini Gabon na Guinea ya Ikweta mwakani litapigwa kesho jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya nyota hao jana walisema uwezo wa Tanzania kuifunga Algeria upo kulingana na mchezo wa awali waliocheza nayo mjini Algers, ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika mjini Algers mwezi Machi mwaka huu Taifa Stars iliilazimisha sare ya 1-1 Algeria ikiwa ugenini.
No comments:
Post a Comment