Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza Gary Neville, amesema timu ya Taifa ya Uingereza isingeweza kutwaa kombe la Dunia mwaka 2010 hata kama Sir Alex Ferguson angekuwa kocha.
Timu ya Taifa ya Uingereza ilitolewa kwenye hatua ya pili ya mashindano hayo yaliyofanyika Afrika Ya Kusini, huku Neville akiendelea kusema kwamba, timu imekosa umoja, nguvu na vipaji halisi toka kwa wachezaji, kitu ambacho kinapelekea kushindwa kufanya vizuri.
Leo timu hiyo leo inaingia uwanjani kucheza na timu ya Taifa ya Bulgaria, kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Bara la Ulaya, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Vasil Levski Stadium, Sofia, kuanzia saa Moja na Robo kwa saa za UK.
No comments:
Post a Comment