Friday, September 2, 2011

Cheka Amtwanga Maugo kwa Pointi

Cheka na Maugo Ulingoni

BONDIA Francis Cheka ‘SMG’ kutoka Morogoro, alimdunda bondia Mada Maugo ‘Mbunge wa Musoma’ katika pambano lisilo la kuwania ubingwa, lililofanyika Mjini Morogoro kwenye uwanja wa Jamuhuri.

Maugo ambaye kabla ya pambano hilo alikuwa akijidadi kuwa atampiga vibaya Cheka kwa kipigo cha mbwa mwizi, alishindwa kutimiza kauli hiyo na badala yake yeye ndie alikumbana na wakati mgumu ulingoni.

Pambano hilo lisilokuwa la ubingwa, lilichezeshwa na waamuzi toka chama cha TPBC ambapo, Jaji wa kwanza alitoa matokeo ya sare kwa mabondia wote yaani  alama 98-98, wakati Jaji wa pili alimpa Cheka ushindi wa alama 99-98, na Jaji wa tatu alimpa Cheka ushindi wa alama 100-98.

No comments:

Post a Comment