Thursday, September 1, 2011

Mikael Arteta Atetea Uamuzi wake Kuhamia Arsenal

Mikael Arteta

Mchezaji mpya wa timu ya Arsenal Mikel Arteta amesisitiza kwamba anaamini hajawaangusha Everton, na hii ni kutokana na kitendo chake cha kushinikiza maombi ya kutaka kuondoka timu hiyo katika dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, ili aweze kufanikisha uhamisho wake.

Inaelezwa kwamba mwanzoni Everton walikataa ofa ya £10m iliyotolewa na Arsenal kwa kiungo huyo, ila mara baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kushinikiza kutaka kuhama, Meneja wa timu ya Everton David Moyes hakuwa na jinsi.

Uhamisho huo ulifanyika muda mchache kabla saa tano kamili kwa saa za Uingereza, muda ambao ndio mwisho wa dirisha la usajili kufungwa, kitu ambacho kiliwacha Everton kuwa na muda mchache wa kuweza kutafuta mbadala wake.

Arteta alimalizia kwa kusema: "Nimejitahidi kuwa mchezaji wa kulipwa kadiri nilivyoweza ila hii ndio soka":

No comments:

Post a Comment