Friday, September 2, 2011

Uholanzi yafanya Mauwaji

Wachezaji wa Uholanzi Wakipongezana

Timu ya taifa ya Uholanzi imejiwekea rekodi yake ya ushindi mkubwa zaidi kuwahi kupata, hii ni baada ya kuifunga San Marino kwa mabao 11-0

Kwa ushindi huo, Uholanzi imeendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya mbio za kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Ulaya hapo mwakani.

Magoli yaliyofungwa na Robin van Persie (4x), Wesley Sneijder (2x), John Heitinga, Klaas-Jan Huntelaar (2x) Dirk Kuyt na Georginio Wijnaldum, yalisaidia kuiwapa vijana hao wa Oranje pointi tatu, kwenye mechi iliyochezwa ndani ya jiji la Eindhoven.

Kufuatia ushindi huu, Uholanzi sasa wamefikisha jumla ya pointi 21 kutokana na michezo saba walizocheza, huku wakiwa nanaongoza Kundi E la Michuano hiyo, na mechi inayofuata watacheza September 6 dhidi ya Finland.

San Marino wanaendelea kukamata mkia kwenye kundi hilo, wakiwa hawana poiti hata moja kwa mechi nane walizocheza, na watakutana na Sweden kwenye mechi itakayofata ikichezwa Jumanne ijayo.


 7′ Robin Van Persie   12′ Wesley Sneijder   17′ John Heitinga   49′ Dirk Kuyt   56′ Klaas-Jan Huntelaar   65′ Robin Van Persie   67′ Robin Van Persie   77′ Klaas-Jan Huntelaar   79′ Robin Van Persie   87′ Wesley Sneijder   90′ Georginio Wijnaldum

No comments:

Post a Comment