Sunday, September 4, 2011

Wilshere Nje ya Uwanja Mpaka November

Jack Wilshere

Mchezaji Chipukizi Nyota wa Arsenal  Jack Wilshere, ataendelea kuwa nje ya dimba kwa miezi miwili zaidi, hii ni kutokana na kutonesha enka yake ya mguu wa kulia.
Wilshere amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi sasa, na hakuwahi kuhusishwa na mechi yoyote ngumu ambayo timu yake ilishiriki toka msimu mpya uanze, na hii ni kutokana na timu hiyo kutotaka kumuwahisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye kwa sasa anavaa kiatu maalumu kwa ajili ya kuulinda mguu wake, ilikuwa tayari imeshaaminika kwamba mwishoni mwa mwezi July angekuwa umepona, ila  aliutonesha mguu kwenye maandalizi ya msimu, ikiwa ni dakika saba tu toka aingie kwenye mechi dhidi ya New York Red Bulls.
Wilshere, akaja tena kupata maumivu mwezi uliopita akiwa mazoezini, maumivu ambayo yaliaminika yangeweza kumuweka nje ya uwanja kwa wiki mbili au tatu, ila sasa imefahamika atakaa nje ya uwanja mpaka mwezi wa November.
Msemaji wa Klabu ya Arsenal amethibitisha: "Atakuwa nje kwa kipindi cha miezi kadhaa, anahitaji kupumzika, na baada ya hapo tutajua wapi kafikia.''

No comments:

Post a Comment