Thursday, September 1, 2011

Tevez Anaweza Endelea Kubaki City

Tevez & Aguero

Mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez, " kwa sasa yupo na furaha kwenye Klabu yake", na kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kubaki na kuitumikia timu hiyo ya Eastlands kwa kipindi kirefu, hii ni kwa mujibu wa muwakilishi wake Kia Joorabchian.

Ujio wa Mke na Watoto wake ndani ya Manchester hivi karibuni, umefuta matamanio ya kutaka kuihama klabu hiyo, na kuna kila sababu za yeye kuweza kubaki, alisema Kia Joorabchian. Na hata uwepo wa mchezaji mwenzake toka nchi yake ya Argentina Sergio Aguero, zinapelekea moja kwa moja kumshawaishi Tevez kubaki Manchester City.

No comments:

Post a Comment