Friday, September 2, 2011

Bendtner: Sirudi Tena Arsenal


Nicklas Bendtner

MUDA mchache baada ya kufanikisha uhamisho wake wa mkopo na kujiunga na Klabu ya Sunderland , mshambuliaji wa Arseanl Nicklas Bendtner amesema hatorudi tena kwenye klabu hiyo ya Emirates.

Kwa kipindi cha miaka sita alichokuwa timu hiyo Bendtner, 23, ameonekana kuwagawa kimawazo mashabiki wengi wa Arsenal, kuna ambao wanaamini ana uwezo na anahitaji kufanikiwa kwa kiwango cha juu na kuna wale wanaomuona sio.

Mchezaji huyo wa kimataifa toka Denmark anaamini alistahili kuwa anaongoza safu ya ushambuliaji wa timu hiyo, ila mwisho wa siku imekuwa ni kinyume kwa kocha wake Arsene Wenger.

Msimu uliopita Bendtner, alipata nafasi chache za kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo na hasa baada ya kupata ajali ya gari miaka miwili iliyopita, na sasa amejiunga na Klabu ya Sunderland kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment