Saturday, September 3, 2011

Kolo Toure Ndani, Hargreaves Nje Kikosi Cha Man City .

Kolo Toure

Klabu ya Manchester City, imetaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki kwenye mashindano ya Kombe la Mabingwa Barani Ulaya, huku kiungo aliyesajiliwa hivi karibuni Owen Hargreaves akienguliwa kwenye kikosi hicho.

Kiungo huyo ameshindwa kujumuishwa kwenye kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa Roberto Mancini licha ya hivi karibuni kusajiliwa na timu hiyo.

Beki Kolo Toure amejumuishwa kwenye kikosi baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi sita kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kutumia madawa.

 Mchezaji mwingine wa timu hiyo Wayne Bridge, ametoswa kwenye kikosi japo haikuelezwa sababu ya kuachwa kwake.

Kikosi Kamili cha Man City Ligi ya Mabingwa :

Makipa: Joe Hart, Costel Pantilimon, Stuart Taylor.

 Mabeki: Gael Clichy, Joleon Lescott, Nedum Onuoha, Micah Richards, Aleksandar Kolarov, Vincent Kompany, Kolo Toure, Pablo Zabaleta, Stefan Savic.

Viungo: Gareth Barry, Adam Johnson, James Milner, Nigel De Jong, Samir Nasri, David Silva, Yaya Toure.

Washambuliaji: Sergio Aguero, Edin Dzeko, Carlos Tevez, Mario Balotelli.

Senegal book place in finals


Senegal secured their place in next year's African Nations Cup with a 2-0 win over DR Congo.
Moussa Sow put Senegal in front in the 35th minute and, although they had a second ruled out for offside before half-time, Sow found the net again in the 52nd minute to secure the points and lock-up qualification.
Senegal join Botswana and Ivory Coast in qualifying for the tournament, while co-hosts Equatorial Guinea and Gabon also have places secured.
Victory for Senegal leaves Cameroon facing an uphill battle to qualify, and they were largely unimpressive against lowly Mauritius before somehow compiling a flattering 5-0 scoreline.
Goals from Leo Kweuke and Matthew Andongcho put them in charge before Samuel Eto'o added a third from the penalty spot.
A late brace from Eric Choupo-Moting gave the Indomitable Lions a margin of victory they scarcely deserved, even before Eyong Enoh's late goal was disallowed for handball.
Defending champions Egypt had their elimination confirmed as a youthful side went down 2-1 to Sierra Leone.
Sheriff Suma got the opening goal in the 14th minute and, although Mohsen Maruwen equalised on the stroke of half-time, Mohamed Bangura's late penalty ended Egypt's campaign.
Sierra Leone move level with South Africa at the top of Group G ahead of the latter's clash with Niger on Sunday.
There was no place for Kolo Toure - eligible again after completing a six-month drugs ban - in the Ivory Coast starting line-up but they did not miss him in a 5-0 demolition of Rwanda in Group H.
The Ivory Coast goals came in a flood, with Salomon Kalou's opener swiftly followed by a quickfire brace from Wilfried Bony that left Rwanda reeling in Kigali.
In the second half, Gervinho teed up Didier Ya Konan for the fourth before getting the fifth himself as the Elephants, who have already qualified, ran riot.
Libya, playing in Egypt under the nation's new flag and in a new kit after the fall of Muammar Gaddafi, recorded a 1-0 win over Mozambique thanks to Reyad Ellafi's 31st-minute goal, sending them top of Group C ahead of Zambia's game against Comores on Sunday.
A goal in the dying minutes from Tangeni Shipahu gave Namibia a 1-0 win over the Gambia, which sees them draw level with their opponents in Group F but effectively hand Burkino Faso qualification as they sit five points clear at the top.
Denis Oliech's late goal gave Kenya a vital 2-1 win over Guinea Bissau in Nairobi.
Needing victory to keep their hopes alive, Kenya had to wait until the hour mark to see Mike Baraza break the deadlock, and then watched as Danilo Luis Pereira lashed home an equaliser in the 89th minute.
But just as hope was fading, Oliech scored in the 92nd minute for secure three points that keep Kenya's qualification hopes alive in Group J.
Uganda can qualify from the group on Sunday with a victory over Angola, who would then face a battle with Kenya for second place.
Cheick Diabate's quick brace put Mali on course for a 3-0 victory over Cape Verde that sent them to the top of Group A. Mahamand Traore made sure of the win in the second half.

In Group D, Tanzania and Algeria did little to help their qualification hopes with a 1-1 draw.
Tanzania took the lead through Mbwana Samata midway through the first half, but Hameur Bouazza fired in an equaliser just before the hour mark, leaving both teams on five points, trailing Morocco and Central African Republic - who clash on Sunday - by two points.
In Group K, Malawi and Tunisia drew 0-0, leaving both teams locked on 11 points in the battle for second place behind Botswana.

Gerrard kurudi dimbani Sept. 18

Steven Gerrard

Mchezaji wa timu ya Liverpool Steven Gerrard, yuko karibu kurudi uwanjani baada ya kuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitano kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamkabili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ameshindwa kuichezea timu Liverpool na timu ya Taifa ya Uingereza toka mwezi wa March kutokana na upasuaji uliofanywa kwenye goti lake.

Anategemea kurudi kwenye mechi ya Ligi kuu ya Uingreza siku ambayo timu yake itakabiliana na Tottenham.

Gerrard ameueleza mtandao Liverpool "Najisikia vizuri sana, nimerudi na kwa sasa naweza hata kupiga mpira, naona mambo sasa yapo sawa. Naamini nitarudi kamili mazoezini siku ya Alhamisi ua Ijumaa."

Gerrard aliongeza: "Sitokuwepo kwenye mechi dhidi ya Stoke Jumamosi ijayo, ila naamini nitahusishwa moja kwa moja kwenye mechi yetu dhidi ya Tottenham, ila bado utabaki kuwa uwamuzi wa Kenny kama naweza kurudi uwanjani ."

"Nimekuwa na mapumziko marefu, nina nguvu na ari tena, najua nitarudi nikiwa fiti, mwenye nguvu na mwenye uchu wa hali ya juu ambao sijawahi kuwa nao". Alisema Gerrard.

Friday, September 2, 2011

Taifa Stars Lazma Kieleweke LEO


Kikosi Cha Stars

KIKOSI cha Taifa Stars kinaingia leo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kupambana na Algeria katika mechi ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika.

Hii ni mechi ya marudiano kwa timu hizi kwa sababu katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja wa Mustafa Tchaker uliopo mjini Blida kilomita 45 kutoka katika mji wa Algiers, Taifa Stars ilitoka sare1-1.

Mpaka sasa kikosi cha Taifa Stars kimepoteza mechi mbili katika mechi nne kilichocheza katika kutafuta nafasi ya kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2012 zitakazofanyika kwenye nchi za Gabon na Guinea ya Ikweta.

Mechi ya mwisho Taifa Stars ilishindwa kutamba mbele ya timu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kuchapwa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Barthelemy Boganda mjini Bangui.

Kutokana na kupoteza mechi hiyo Taifa Stars hivi hivi sasa ipo katika nafasi ngumu ya kufuzu kushiriki fainali hizo za Afrika, ambapo imebakisha mechi mbili ambazo inatakiwa kushinda mechi zote ili ifikishe pointi 10 kuweza kufuzu.

Taifa Stars imebakisha mechi dhidi ya Algeria ambayo inachezwa leo jijini Dar es Salaam, pia imebakisha mechi dhidi ya Morocco ambayo itachezwa huko mjini Rabat kwenye uwanja wa Prince Moulay Abdellah kati ya tarehe 7,8,9/10/2011.

Mpaka sasa Taifa Stars imeshinda mechi moja ambayo iliifunga Jamhuri ya Afrika ya Kati mabao 2-1 katika pambano lililopigwa jijini Dar es Salaam, ilitoka sare ya bao 1-1 na Algeria, vile vile Stars ilifungwa bao 1-0 na Morocco kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mechi ilizocheza Taifa Stars hivi sasa inashika nafasi ya tatu katika kundi D ikiwa na pointi nne sawa na Algeria inayoshika nafasi ya nne ikiwa na pointi nne, timu inayoshika nafasi ya kwanza katika kundi hilo ni Morocco yenye pointi saba ikifuatiwa na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo ina pointi saba pia.

Morocco yenyewe hivi sasa imebakisha mechi dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mechi itakayochezwa mjini Bangui pia imebakisha mechi dhidi ya Tanzania itakayochezwa mjini Rabat, wakati Jamhuri ya Afrika ya Kati imebakisha mechi dhidi ya Morocco mjini Bangui na mechi dhidi ya Algeria huko nchini Algeria.

Algeria pia imebakisha mechi ya leo dhidi ya Tanzania mjini Dar es Salaam na mechi dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati huko nchini Algeria.

Kama Morocco ikishinda mechi zote itafikisha pointi 13 na Jamhuri ya Afrika ya Kati ikishinda mechi zote itafikisha pointi 13 , hivyo Taifa Stars ina kazi kubwa ya kufanya, vile vile inatakiwa kuomba Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati zifanye vibaya katika mechi zilizobakia.

Ni wazi wachezaji wetu waliochaguliwa na kocha Poulsen kuunda kikosi cha timu ya taifa hivi sasa wana kazi kubwa ya kulivusha taifa la Tanzania katika kipindi hiki kigumu ili tuweze kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2012.

Wachezaji wa Stars leo wanatakiwa kuingia uwanjani wakiwa na lengo moja tu la kupata ushindi siyo kutoka sare wala kufungwa.

Tunafahamu mchezaji wa timu ya taifa kazi yake ni kupigania kitu ambacho huwa na thamani na kumbukumbu kubwa kwa vizazi vingi vitakavyofuatia.

Kitu wanacholeta wachezaji wa timu ya taifa ni ushindi, siku zote wachezaji wa timu ya taifa wanaposhinda huwa wanaliletea taifa lao furaha na kujisikia fahari kuishi katika taifa hilo, hivyo tunatarajia wachezaji waliochaguliwa na kocha Jan Poulsen wataweza kutuletea furaha wananchi wa Tanzania katika mechi ya leo.

Tunaamini wachezaji wa Stars watatumia akili ya mchezo kwa ahali ya juu, nguvu na stamina waliyonayo ili kupata ushindi leo.

UEFA Euro 2012 Qualifying Results

Rooney & Terry

Group A

Germany remain perfect in their qualifying campaign (8 for icon cool UEFA Euro 2012 Qualifying Results with a very comfortable win over Austria, 6-2, at Gelsenkirchen. Mesut Ozil scored a hat trick, with Lukas Podolski, Andre Schurrle and Mario Gotze doing the rest. The Germans were up 3-0 in less than 28 minutes, but a goal from Marko Arnautovic cooled them off for a short while. Martin Harnik scored the second for Austria.
Turkey beat Kazakhstan 2-1 with a deep deep injury time goal by Arda Turan. Belgium were held to a costly 1-1 draw at Baku against Azerbaijan. 
Gemrnay, with 24 points after 8 matches, are clear and set in the 2012 Euros. Turkey are second with 13 points after seven games played, Belgium are third with 12 points and eight games played. Both still have to face the Germans.

Group B

Still very tight in the group – Ireland were held at home to a 0-0 draw against Slovakia, Armenia beat Andorra 3-0 in Andorra while Russia squeezed out a 1-0 win over Macedonia in Moscow with a goal from Igor Semshov, the 33 year old from Dynamo Moscow.
All nations have played 7 matches – Russia lead the group with 16 points, Ireland and Slovakia with 14 and Armenia still in the mix with 11 points. Ireland play in Moscow on Tuesday while Armenia visit Slovakia.

Group C

Italy nearly secure their place in the tournament with a 1-0 win in the Faroe Islands with an early Antonio Cassano goal. Estonia stunned Slovenia in Ljubljana with goals from Konstantin Vassilijev and Ats Purje. Serbia earned a crucial 1-0 win over Northern Ireland through Marko Pantelic.
Italy lead the group with 19 points, but it’s all tight from there – Slovenia (8 matches) have 11 points, Serbia have 11 but a game less, Estonia (8) have 10 points and Northern Ireland (7) have 9 points.

Group D

France remain in control of the group with a 2-1 win in Tirana against Albania with goals from Karim Benzema (his 13th goal for France and 3rd in these qualifiers) and Yann M’Vila. Bosnia won 2-0 in Belarus with goals from Sejad Salihovic and Haris Medunjanin. Romaina grabbed a 2-0 victory against Luxemborg with two goals from Gabriel Torje (Udinese).
France lead the group with 13 points in six matches. Bosnia have 13 in 7, Belarus have 12 in 8 and Romania have 11 in 7.

Group E

The Netherlands didn’t hold back against amateurish (at best) San Marino winning 11-0, remaining perfect on their easy road towards Poland and the Ukraine. Robin van Persie forgot his Arsenal woes, scoring four goals, making it six for him in these qualifiers. Wesley Sneijder and Klaas Jan Huntelaar scored two each. Hungary got a huge win over Sweden through a 90th minute goal from Gergely Rudolf, getting the 2-1 win. Finalnd beat Moldova 4-1.
The Dutch have 21 points in 7 matches. Sweden have 15 from 7 while Hungary have 15 from 8. Sweden still have to play the Dutch again (in Sweden), but they do win the tie breaker with Hungary thanks to their 2-0 win at home.

Group F

Greece got a big win in Israel, 1-0 through Sotiris Ninis, leaving Israel hardly a chance to qualify from the group. Croatia got a 3-1 win in Malta and Latvia beat Georgia 1-0. Greece have 17 points after 7 matches, Croatia are with 16 at second. The Greeks host Croatia next month.

Group G

England remained perfect away from Wembley, beating Bulgaria 3-0 with goals from Gary Cahill and Wayne Rooney (2), reaching 28 for the national team. Wales did England a huge favor with their first win of the qualifiers, beating Montenegro 2-1 in Cardiff through Steve Morison and Aaron Ramsey.
England lead the group with 14 points after six matches, Montenegro are second with 11.

Group H

Things are still rather complicated in this one, with three nations in the picture. Group leaders Portugal won 4-0 in Cyprus, with Cristiano Ronaldo scoring twice, taking him to 29 international goals and four in these qualifiers. Norway got a late penalty to give them a 1-0 win over Iceland, scored by Mohammed Abdellaoue. 
Portugal have 13 points at first, same as Norway. Both teams beat each other 1-0 in their home matches. Denmark are third with 10 points and 5 matches. They host Norway on Tuesday and host Portugal next month.

Group I

Only one match played today – Lithuania drew Lichtenstein without any goals. Spain lead the group with 15 points (100%), the Czech Republic, playing in Scotland tomorrow, are second with 9 points. Scotland have only 4 points at fourth after four matches, and can’t afford not to win at Hampden Park tomorrow if they want to have a chance of finishing second.

Ujerumani ya Kwanza Kutinga UEFA EURO 2012


Wachezaji wa Ujerumani Wakipongezana

Germany 6 vs 2 Austria
Ujerumani imekuwa nchi ya kwanza kufaulu kuingia kwenye Fainali za UEFA EURO 2012, na hii ni baaada ya ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Austria.

Magoli ya Ujerumani yalifungwa na  8′ Miroslav Klose, 23′ Mesut Özil, 28′ Lukas Podolski,  47′ Mesut Özil,   84′ Andre Schürrle na 89′ Mario Götze. Wakati yale ya Austria yalifungwa na  
 Marko Arnautovic 42′ na Martin Harnik 51′

Chicharito Asawazisha Poland vs Mexico

Javier 'Chicharito' Hernandez

Mchezaji wa timu ya Manchester United, Javier 'Chicharito' Hernandez, amerejea tena uwanjani kuichezea timu ya Taifa lake la Mexico, na kuweza kuisaida kutoka sare1-1 dhidi ya Poland,

Chicharito aliweza kuisaidia timu hiyo, baada ya kufunga goli la kusawazisha lililopelekea mechi hiyo kuisha kwa sare.

Hii ilikuwa ni mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Pepsi Arena kwenye jiji la Warsaw

Uholanzi yafanya Mauwaji

Wachezaji wa Uholanzi Wakipongezana

Timu ya taifa ya Uholanzi imejiwekea rekodi yake ya ushindi mkubwa zaidi kuwahi kupata, hii ni baada ya kuifunga San Marino kwa mabao 11-0

Kwa ushindi huo, Uholanzi imeendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya mbio za kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Ulaya hapo mwakani.

Magoli yaliyofungwa na Robin van Persie (4x), Wesley Sneijder (2x), John Heitinga, Klaas-Jan Huntelaar (2x) Dirk Kuyt na Georginio Wijnaldum, yalisaidia kuiwapa vijana hao wa Oranje pointi tatu, kwenye mechi iliyochezwa ndani ya jiji la Eindhoven.

Kufuatia ushindi huu, Uholanzi sasa wamefikisha jumla ya pointi 21 kutokana na michezo saba walizocheza, huku wakiwa nanaongoza Kundi E la Michuano hiyo, na mechi inayofuata watacheza September 6 dhidi ya Finland.

San Marino wanaendelea kukamata mkia kwenye kundi hilo, wakiwa hawana poiti hata moja kwa mechi nane walizocheza, na watakutana na Sweden kwenye mechi itakayofata ikichezwa Jumanne ijayo.


 7′ Robin Van Persie   12′ Wesley Sneijder   17′ John Heitinga   49′ Dirk Kuyt   56′ Klaas-Jan Huntelaar   65′ Robin Van Persie   67′ Robin Van Persie   77′ Klaas-Jan Huntelaar   79′ Robin Van Persie   87′ Wesley Sneijder   90′ Georginio Wijnaldum

Fergie na Dzeko Watwaa Tuzo za Mwezi Barclays


Sir Alex Ferguson

Kocha wa timu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson, ametangazwa kuwa Meneja wa mwezi Barclays Premier League kwa mwezi wa nane, hii ikiwa ni mara ya 26 kwake kushinda tuzo.

Na kwa upande mwingine Mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko, amechaguliwa mchezaji bora wa mwezi wa August na kushinda Tuzo hiyo upande wa wachezaji .

Mchezaji Mpya wa Arsenal Mkorea Park Chu-Young apiga Hat-Trick

Park Chu-Young

Mchezaji mpya wa Arsenal Park Chu-Young, mchana wa leo ameiwezesha Nchi yake Korea Kusini kupata ushindi a magoli 6-0 dhidi ya Lebano.

Katika mchezo Park Chu-Young aliweza kufunga magoli matatu (hat-trick), huku magoli mengine yakifungwa na mshambuliaji mpya wa timu ya Sunderland Ji Dong-Won, huku mengine mawili yakifungwa na kiungo wa Timu ya Sangju Sangmu  Kim Jung-Woo.

Kwa ushindi huo Korea Kusini, imejiweka kwenye mwanzo mzuri wa kampeni yake, kuweza kupata tiketi ya kushiriki kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Bendtner: Sirudi Tena Arsenal


Nicklas Bendtner

MUDA mchache baada ya kufanikisha uhamisho wake wa mkopo na kujiunga na Klabu ya Sunderland , mshambuliaji wa Arseanl Nicklas Bendtner amesema hatorudi tena kwenye klabu hiyo ya Emirates.

Kwa kipindi cha miaka sita alichokuwa timu hiyo Bendtner, 23, ameonekana kuwagawa kimawazo mashabiki wengi wa Arsenal, kuna ambao wanaamini ana uwezo na anahitaji kufanikiwa kwa kiwango cha juu na kuna wale wanaomuona sio.

Mchezaji huyo wa kimataifa toka Denmark anaamini alistahili kuwa anaongoza safu ya ushambuliaji wa timu hiyo, ila mwisho wa siku imekuwa ni kinyume kwa kocha wake Arsene Wenger.

Msimu uliopita Bendtner, alipata nafasi chache za kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo na hasa baada ya kupata ajali ya gari miaka miwili iliyopita, na sasa amejiunga na Klabu ya Sunderland kwa mkopo.

Nyota Stars: Hakika Kitaeleweka


Nizar Khalfan

Wachezaji Nyota wa Tanzania wanaokipiga nje ya nchi wamewataka mashabiki na wadau wote wa soka kujitokeza kwa wingi kesho kwenye Uwanja wa Taifa na kuwapa sapoti ya kutosha kwani wamekuja kivingine na kuahidi ushindi mkubwa dhidi ya Algeria.

Nyota hao saba ni Nizar Khalfan (Vancouver WhiteCaps, Canada), Danny Mrwanda na Abdi Kassim (Don Long, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Henry Joseph, Athuman Machupa na Idrissa Rajabu (Sofapaka, Kenya).

Pambano hilo la kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika nchini Gabon na Guinea ya Ikweta mwakani litapigwa kesho jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti baadhi ya nyota hao jana walisema uwezo wa Tanzania kuifunga Algeria upo kulingana na mchezo wa awali waliocheza nayo mjini Algers, ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1. 

 
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika mjini Algers mwezi Machi mwaka huu Taifa Stars iliilazimisha sare ya 1-1 Algeria ikiwa ugenini.

Cheka Amtwanga Maugo kwa Pointi

Cheka na Maugo Ulingoni

BONDIA Francis Cheka ‘SMG’ kutoka Morogoro, alimdunda bondia Mada Maugo ‘Mbunge wa Musoma’ katika pambano lisilo la kuwania ubingwa, lililofanyika Mjini Morogoro kwenye uwanja wa Jamuhuri.

Maugo ambaye kabla ya pambano hilo alikuwa akijidadi kuwa atampiga vibaya Cheka kwa kipigo cha mbwa mwizi, alishindwa kutimiza kauli hiyo na badala yake yeye ndie alikumbana na wakati mgumu ulingoni.

Pambano hilo lisilokuwa la ubingwa, lilichezeshwa na waamuzi toka chama cha TPBC ambapo, Jaji wa kwanza alitoa matokeo ya sare kwa mabondia wote yaani  alama 98-98, wakati Jaji wa pili alimpa Cheka ushindi wa alama 99-98, na Jaji wa tatu alimpa Cheka ushindi wa alama 100-98.

Milan Wamtema Inzaghi Kwenye Kikosi Cha Ligi Ya Mabingwa Ulaya


Filippo Inzaghi

Mshambuliaji mkongwe wa timu ya AC Milan Filippo Inzaghi, ametemwa kwenye kikosi cha AC Milan kitakachoshiriki kwenye Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya msimu huu, hii inamfanya Inzaghi ashindwe kuvunja rekodi ya ufungaji wa mabao inayoshikiliwa na Raul kwa sasa.

Akiwa amecheza mechi 115 na kufunga magoli 70, Inzaghi anaendelea kuwa nyuma ya Raul ambaye mpaka sasa amemtangulia kwa magoli mawili zaidi, Raul ambaye ni mmoja kati ya wachezaji wanaoheshimika na Real Madrid, ana jumla ya magoli 72 katika michuano hiyo.

Na kwa umri wa miaka 38 alionao Inzaghi, inaonyesha moja kwa moja mchezaji huyo tamati yake ndio imefika, na itakuwa ngumu kuweza kulinyakua tena taji ambalo Raul alilipora kwake msimu uliopita.

Msimu uliopita kwenye ligi hiyo Raul alifunga magoli matano akiwa na timu ya Schalke ya nchini Ujerumani, na kuweza kumpiku gwiji huyo aliyekuwa anaongoza kwa kipindi kirefu.

Neville: Uingereza Isingechukua Kombe La Dunia Hata Ferguson Angekuwa Kocha



Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza Gary Neville, amesema timu ya Taifa ya Uingereza isingeweza kutwaa kombe la Dunia mwaka 2010 hata kama Sir Alex Ferguson angekuwa kocha.
Timu ya Taifa ya Uingereza ilitolewa kwenye hatua ya pili ya mashindano hayo yaliyofanyika Afrika Ya Kusini, huku Neville akiendelea kusema kwamba, timu imekosa umoja, nguvu na vipaji halisi toka kwa wachezaji, kitu ambacho kinapelekea kushindwa kufanya vizuri.

Leo timu hiyo leo inaingia uwanjani kucheza na timu ya Taifa ya Bulgaria, kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Bara la Ulaya, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Vasil Levski Stadium, Sofia, kuanzia saa Moja na Robo kwa saa za UK.

Thursday, September 1, 2011

Tevez Anaweza Endelea Kubaki City

Tevez & Aguero

Mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez, " kwa sasa yupo na furaha kwenye Klabu yake", na kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kubaki na kuitumikia timu hiyo ya Eastlands kwa kipindi kirefu, hii ni kwa mujibu wa muwakilishi wake Kia Joorabchian.

Ujio wa Mke na Watoto wake ndani ya Manchester hivi karibuni, umefuta matamanio ya kutaka kuihama klabu hiyo, na kuna kila sababu za yeye kuweza kubaki, alisema Kia Joorabchian. Na hata uwepo wa mchezaji mwenzake toka nchi yake ya Argentina Sergio Aguero, zinapelekea moja kwa moja kumshawaishi Tevez kubaki Manchester City.

Kikosi Cha Wachezaji XI Waliosajiliwa EPL

Dirisha la Usajili limefungwa rasmi jana saa 5 Usiku kwa saa za Uingereza, na litafunguliwa tena mwezi January likifahamika kama dirisha Dogo. Kwa mtazamo wake, Mchambuzi wa BBC Sports Mark Lawrenson ametaja listi ya wachezaji 11, na hawa ni wachezaji waliosajiliwa katika kipindi cha usajili toka vilabu vya nje ya Uingereza, na hii hapa ndio Starting XI yake.


Upi Mtazamo wako?
Toa maoni yako kwa kubofya hapo chini palipoandikwa comments

Pereira Naheshimu Maamuzi ya Porto

Alvaro Pereira

Alvaro Pereira amesisitiza kwamba anaheshimu maamuzi ya timu yake ya Porto ya kukataa ofa ya Klabu ya Chelsea ya kutaka kumsajili yeye.

Chelsea walijaribu mpaka siku ya mwisho kumnasa winga huyo toka Uruguay ikashindikana, mchezaji huyo pia anaweza kucheza nafasi ya kiungo.

Porto walikuwa wanahitaji kiasi cha £25m toka kwa kocha wa zamani wa timu hiyo Andre Villas-Boas, ambaye kwa sasa ni kocha wa Chelsea, ili aweze kuungana tena na mchezaji huyo pande za Stamford Bridge.

Dau hilo likaonekana kubwa na Chelsea wakashindwa kufikia matakwa ya Porto, hivyo kumfanya Pereira aendelee kubaki na mabigwa hao wa Europa League.

"Klabu ilikataa hiyo ofa, nami nitaendelea kuwa kwenye rangi za Porto” Pereira aliieleza Sport 890 ya Uruguay.

"Walisema hawakutaka kuniuza na kuidhohofisha timu, na mimi kama mchezaji sina budi kuheshimu maamuzi.

"Chelsea walichoshwa na hiyo hali ikabidi wajitoe. Wakala wangu alinieleza kwamba timu hizi mbili zimeshindwa kufikia makubalianao.

"Nahitaji kujikita zaidi na Porto kwa sasa huku nikijaribu kuwa na mcheza mzuri, itakuwa sio rahisi ila hiyo ni changamoto kwangu." Alisema Pereira.

Ilielezwa kwamba Chelsea walikuwa wapo tayari kutoa ofa ya €20m, wakianza kwanza kutoa €10m kwa mchezaji huyo.

Mikael Arteta Atetea Uamuzi wake Kuhamia Arsenal

Mikael Arteta

Mchezaji mpya wa timu ya Arsenal Mikel Arteta amesisitiza kwamba anaamini hajawaangusha Everton, na hii ni kutokana na kitendo chake cha kushinikiza maombi ya kutaka kuondoka timu hiyo katika dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, ili aweze kufanikisha uhamisho wake.

Inaelezwa kwamba mwanzoni Everton walikataa ofa ya £10m iliyotolewa na Arsenal kwa kiungo huyo, ila mara baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kushinikiza kutaka kuhama, Meneja wa timu ya Everton David Moyes hakuwa na jinsi.

Uhamisho huo ulifanyika muda mchache kabla saa tano kamili kwa saa za Uingereza, muda ambao ndio mwisho wa dirisha la usajili kufungwa, kitu ambacho kiliwacha Everton kuwa na muda mchache wa kuweza kutafuta mbadala wake.

Arteta alimalizia kwa kusema: "Nimejitahidi kuwa mchezaji wa kulipwa kadiri nilivyoweza ila hii ndio soka":

Sneijder: Najisikia Furaha Kubaki Inter

Wesley Sneijder kwenye Mahojiano na AD

Mchezaji wa Inter Milan Wesley Sneijder ameebainisha kwamba alikuwa karibu kujiunga na Manchester United, ila akasisitiza anajisikia furaha kubaki Inter.

Sneijder amehusishwa na mpango wa kuhamia Old Trafford katika kipindi chote cha majira ya joto.

"Nilihisi uhamisho wangu kwenda Man U uko karibu," Sneijder aliieleza AD. "kulikuwa na mazungumzo kwa mara kadhaa. Ukweli ni kwamba Inter ilikuwa inahitaji kuuza wachezaji, ilikuwa awe Eto'o au mimi. Nia ilikuwepo, ila kutokana na mkanganyiko wa mambo haikuwezekana"

Akaendelea kwa kuongeza "Wao ni moja kati ya klabu kubwa Duniani, kwa hiyo haikuwa mbaya kwangu kujiunga nao, ila kwa kipindi hicho hicho sikuwa nataka kuondoka Inter. Nipo Italia na na kwangu hicho ni kitu kikubwa sana"

Moja kati ya sababu zilizofanya mpango huu kutokamilika ni ishu ya mshahara wa mchezaji huyo kuwa mkubwa, na juu ya hilo Sneijder akasema "Kwangu mimi haikuwa hasa ni ishu ya mkwanja, hapa Inter mambo ni mazuri, naipenda hii Klabu, watu wa Italia na utamaduni wao unaendana na mimi"