Wednesday, August 31, 2011

Dirisha la Usajili Ulaya Lafungwa

Mikel Arteta - Everton to Arsenal, undisclosed
Craig Bellamy - Manchester City to Liverpool, undisclosed
Peter Crouch - Tottenham to Stoke, undisclosed
Raul Meireles - Liverpool to Chelsea, undisclosed
Shaun Wright-Phillips - Manchester to QPR, undisclosed
Wilson Palacios - Tottenham to Stoke City, undisclosed
Alan Hutton - Tottenham to Aston Villa, undisclosed
Jermaine Jenas - Tottenham to Aston Villa, season loan
Yossi Benayoun - Chelsea to Arsenal, season loan
Cameron Jerome - Birmingham to Stoke City, undisclosed
Scott Dann - Birmingham to Blackburn, undisclosed
Per Mertesacker - Werder Bremen to Arsenal, undisclosed
Owen Hargreaves - Manchester City, free
Scott Parker - West Ham to Tottenham, undisclosed
Andre Santos - Fenerbahce to Arsenal, undisclosed
Joe Cole - Liverpool to Lille, season loan
Christian Poulson - Liverpool to Evian, undisclosed
David N'gog - Liverpool to Bolton, undisclosed
Gael Kakuta - Chelsea to Bolton, five-month loan
Shaun Maloney - Celtic to Wigan, undisclosed
Brian Ruiz - FC Twente to Fulham, undisclosed
Orlando Sa - Porto to Fulham, undisclosed
Anton Ferdinand - Sunderland to QPR, undisclosed
Royston Drenthe - Real Madrid to Everton, season loan
Denis Stracqualursi - Tigres to Everton, season loan
Darnel Situ - Lens to Swansea, £250,000
Badr El Kaddouri - Dynamo Kiev to Celtic, five-month loan
Pablo Ibanez - West Brom to Birmingham, undisclosed
Fede Bessone - Leeds to Swansea, free
Zdenek Grygera - Juventus to Fulham, free transfer
Tommaso Trani - Milan to QPR, free agent
Henri Lansbury - Arsenal to West Ham, season loan
Guy Demel - Hamburg to West Ham, free
Liam Feeney - Bournemouth to Millwall, undisclosed
Patrick van Aaanholt - Chelsea to Wigan, season loan
John Guidetti - Manchester City to Feyenoord, season loan
Enda Stevens - Shamrock Rovers to Aston Villa, from Jan 2012
Villyan Bijev - California Odyssey to Liverpool, undisclosed
James Hurst - West Brom to Blackpool, season loan
Daniel Bogdanovic - Sheffield United to Blackpool, undisclosed
Joe Garner - Nottingham Forest to Watford, undisclosed
Dany N'Guessan - Leicester to Millwall, undisclosed
Ben Turner - Coventry City to Cardiff City, undisclosed
Alassane N'Diaye, Crystal Palace, released
Mark Beevers - Sheff Wed to MK Dons, four-month loan
Giles Coke - Sheff Wed to Bury, two-month loan
Anthony McNamee - Norwich to MK Dons, free
Callum Tapping - Tottenham to Hearts, undisclosed
Kelvin Langmead - Peterborough to Northampton, five-month loan
Keammar Daley - Tivoli Gardens to Preston, undisclosed
Tom Adeyemi - Norwich City to Oldham, five-month loan
Ahmed Abdulla, West Ham to Swindon Town, six-month loan
Jed Wallace - Lewes to Portsmouth, undisclosed
Michael Smith - Darlington to Charlton, undisclosed
Emile Sinclair - Macclesfield to Peterborough, undisclosed
Max Gradel - Leeds to St Etienne, undisclosed
Mike Grella - Leeds to Brentford, undisclosed
Peter Ramage - QPR to Crystal Palace, five-month loan
Ryan McGivern - Man City to Bristol City, season loan
Matt Duke - Bradford, free
Jay Simpson - Hull to Millwall, four-month loan
Martyn Waghorn - Leicester to Hull, four-month loan
Michael Timlin - Swindon to Southend, four-month loan
Brett Williams - Reading to Rotherham, five-month loan
Simon King - Gillingham to Plymouth, one-month loan
Damien Mozika - Bury to Scunthorpe, undisclosed
Shaun Harrad - Northampton to Bury, undisclosed
Jamie Griffiths - Ipswich to Plymouth, one-month loan
Andrew Little - Rangers to Port Vale, five-month loan
Jamie Devitt - Hull to Bradford, five-month loan
Shane Byrne - Leicester to Bury, one-month loan
Tom Collins - Stevenage to Hayes and Yeading, one-month loan
Mitchell Nelson - Bournemouth to Lincoln, one-month loan
Peter Winn - Stevenage to Cambridge United, three-month loan
Terry Dixon - Bradford City to Halifax, one-month loan
Ben Swallow - Bristol Rovers to Bath City, three-month loan
John Fleck - Rangers to Sheffield United, season loan
Kyle Hutton - Rangers to Sheffield United, season loan
Mohamadou Sissoko - Udinese to Kilmarnock, season loan
Jude Winchester - Linfield to Kilmarnock, undisclosed
Michael Paton - Aberdeen to Stockport, four-month loan
Ross McKinnon - Motherwell to Dumbarton, one-month loan
Steven Howarth - Motherwell to Alloa, one-month loan
Ryan Connolly - Derby to Ayr, three-month loan

Raul Meireles wa Liverpool ahamia Chelsea

Raul Meireles

Kiungo wa Liverpool Raul Meireles, amefanya uhamisho wa aina yake na kujiunga Chelsea kwa thamani ya £12m.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alituma maombi ya kuhama Anfield muda mfupi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, na ameweza kuingia mkataba wa miaka minne na watoto wa darajani.

Meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas aliwahi kufanya kazi sambamba na mchezaji huyo walipokuwa Porto kabla ya mchezaji huyo kuelekea Anfield mnamo mwezi August mwaka jana.

Meireles kwa sasa ni majeruhi, baada ya kuumia kwenye mechi ya Liverpool ilipocheza na Exeter City kwenye kombe la Carling mapema wiki iliyopita.

Mwanzoni Liverpool waliikataa ofa ya Chelsea kwa mchezaji huyo, ambapo walikuwa wapo tayari kutoa £8m sambamba na Yossi Benayoun ili kuweza kumpata.

Arsenal Yawasajili Mikel Arteta, Yossi Benayoun na Per Mertesacker


Mikel Arteta

Klabu ya Arsenal imemsajili beki wa Everton Mikel Arteta kwa kiasi cha £10m,  hii ni baada ya mchezaji huyo kutuma maombi ya kuhama.

Kiungo huyo wa ki-spania amejiunga na washika bunduki hao kwa mkataba wa miaka minne, na hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya dirisha la usajili kufungwa saa tano kamili kwa saa za Uingereza.

Arsenal pia imefanikiwa kumpata kwa mkopo mchezaji wa Chelsea Yossi Benayoun, kwa msimu mmoja.

Benayoun, ambaye ni nahodha wa nchi yake ya Israel, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema "Nimesajili na Arsenal, nina furaha sana na kupendezwa na jambo hili, ila kwa sasa kichwa changu kinafikiria juu ya mechi dhidi ya Ugiriki hapo Ijumaa, asanteni kwa ushirikiano wenu."

Klabu zote mbili zimethibitisha juu ya maafikiano hayo.

Pia imefahamika kwamba Arsenal wamekamilisha usajili wa Beki wa kimataifa wa Ujerumani Per Mertesacker toka Werder Bremen.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, inaaminika amewagarimu washika bunduki wa Emirates kiasi cha  £8m huku akiwa amesaini mkataba wa muda mrefu.

"Nilikuwa na wakati mzuri na Werder, hakika nawaheshimu sana, ila kuhamia London ni kama ndoto iliyokuwa kweli," alisema Mertesacker huku akiongeza "Kwangu mimi English Premier League mara zote naiona ina mvuto ikiwa na ushindani wa hali ya juu"

Meneja wa timu hiyo Arsene Wenger aliieleza kwenye mtandao wa timu hiyo: "Tumefurahi kumkaribisha Per Mertesacker kwenye Klabu yetu."

Bellamy Arejea Liverpool

Craig Bellamy

Klabu ya Liverpool imethibitisha kumsajili mchezaji aliyewahi kuichezea timu hiyo Craig Bellamy.



Mchezaji huyo ambaye ni nahodha wa Wales, amerudi tena Anfield kwa mkataba wa miaka miwili baada kuwa huru toka Manchester City.

Bellamy ambaye aliondoka Liverpool baada ya msimu wa 2007 na kujiunga na West Ham, inaaminika atasaidia kuongeza nguvu ya ushambuliaji kwenye kikosi cha Kenny Dalglish, akiwa mchezaji wa ziada nyuma ya Luis Suarezna Andy Carroll.

Mbwana Samatta: TP Mazembe ni Shughuli

Mbwana Samatta

Mshambuliaji wa timu ya taifa ‘Taifa Stars Mbwana Samatta anayekipiga na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesema ushindani wa namba katika kikosi cha timu hiyo ni mkubwa sana, na nafasi anayocheza inawaniwa na washambuliaji watano toka mataifa yanayotambulika kisoka Duniani.

Spurs yakataa £40m za Chelsea kumsajili Modric

Luca Modric

Tottenham wamekataa ofa iliyotolewa na timu ya Chelsea ya £40 million, kwa ajili ya kumsajili kiungo wao Luka Modric, hii ni kwa mujibu wa meneja wa timu hiyo Harry Redknapp.

Ngog ajiunga na Bolton


David Ngog

Klabu ya Liverpool imethibitisha kwamba mchezaji wao David Ngog amejiunga na timu ya Bolton kwa mkataba wa miaka mitatu.

Ngog, 22, alijiunga na Liverpool kutoka Paris St Germain mnamo July 2008, amefanikiwa kucheza mechi 94 na kufunga magoli 19, ila alishindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, na hasa baada ya kuwasili kwa Luis Suarez na Andy Carroll mwezi January mwaka huu.

Taarifa kwenye mtandao wa Liverpool imesema: ''Kila mmoja hapa Liverpool FC anamtakia David kheri kwenye taaluma na maisha yake ya mbele.''

Manchester City yamsajili Owen Hargreaves



Manchester City imekamilisha usajili wa aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Owen Hargreaves kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Diego Forlan ajiunga na Inter Milan


Diego Forlan

Klabu ya Inter Milan imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Forlan

Forlan, 32, amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo, ikiaminika ujio wake ni kwa ajili ya kuziba pengo liliachwa na Samuel Eto'o.

''Diego, anakaribishwa Inter,'' inasoma taarifa kwenye mtandao wa klabu ya Inter.

Arsenal yamsajili Andre Santos


Andre Santos

Klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa imemsajili beki wa ki-brazil Andre Santos toka klabu ya Fenerbahce kwa gharama ya Dolla Millioni 6.

Santos, mwenye miaka 28, anategemea kuongeza uzoefu kwenye kikosi cha Arsenal kilicho na wachezaji wengi makinda, inaaminika amesajiliwa ili kuweza kuziba pengo lililoachwa wazi na Gael Clichy, ambae alijiunga na timu ya Manchester City mnamo mwezi July.

Beki huyo ambaye pia amewahi kuichezeea timu ya Corinthians, amesema amefurahi kujiunga kwenye Ligi Kuu ya Uingereza akiwa amefata nyayo za wa Brazil wenzake kama Eduardo, Sylvinho, Denilson na Gilberto Silva ambao wamewahi kichezea Arsenal.

Scott Parker ajiunga Tottenham

Scott Parker

Klabu yaTottenham imefikia makubaliano ya kumsaini kiungo wa Uingereza Scott Parker toka West Ham.

Uhamisho huo, umekuja baada ya mchezaji huyo kuuandikia barua Uongozi wa West Ham juu ya nia yake ya kuhama klabu hiyo. Parker aliandinika, ningetamani nicheze kwenye Ligi kuu.

Ikumbukwe West Ham kwa sasa haipo kwenye Ligi Kuu ya Uingereza na hii ni baada ya kushuka daraja msimu uliopita.

Kiungo wa Liverpool Joe Cole Ajiunga na Lille kwa Mkopo


Joe Cole

Kiungo wa Liverpool Joe Cole, amejiunga na timu Lille ya Ufaransa kwa Mkopo ambao utamuweka huko kipindi chote cha msimu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 jana Jumanne alisafiri kwenda Ufaransa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya, inaelezwa kuwa Aston Villa nao walikuwa wanamtolea macho mchezaji huyo

Chelsea yakaribia kumnasa Pereira

Alvaro Pereira

Wakala wa mchezaji Alvaro Pereira anayekipiga na timu ya Porto, amesema wako kwenye mazungumzo na timu ya Chelsea juu uwezekano wa kumsajili mchezaji wake.

Bosi wa timu ya Blues Andre Villas-Boas anamfahamu vyema mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay toka kipindi walichokuwa pamoja cha Estadio do Dragao wakiwa na timu ya Porto, na sasa anataka kuungana tena na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Mchezaji huyo aliyewahi kuchezea CFR Cluj na Argentinos Juniors, kwa sasa anasubiri kusikia kiasi cha fedha kitakachopitishwa ili aweze kukamilisha usajili wake, na wakala wake Alejandro Savich kwa sasa yupo nchini Uingereza akishughulikia suala hilo.

Timu kama Barcelona, AC Milan na Inter Milan nazo zimetajwa kumtaka mchezaji huyo.

Hii ni mara ya pili kwa Chelsea kutaka kumsajili mchezaji huyo, baada ya maombi yao ya mara ya kwanza kutolewa nje.

Liverpool yakamilisha usajili wa Sebastian Coates

Sebastian Coates

Liverpool wamekamilisha usajili wa Beki wa Kimataifa wa Uruguay Sebastian Coates toka timu ya Nacional ya nchini humo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ni mmoja kati ya wachezaji waliovutia kwenye kikosi cha Uruguay, ambapo aliiwezesha nchi yake kutwaa kombe la Copa mnamo mwezi July mwaka huu, haijaelezwa Coates amaesaini mkataba wa muda gani ila inaaminika amesaini mkataba wa muda mrefu na wana hao wa Anfiel.

Mchezaji huyo beki wa kati mwenye urefu wa nchi 6, amefaulu vipimo vya afya na pia ameweza kupata kibali cha kufanya kazi na timu ya Liverpool, kumfanya awe mchezaji wa 6 kusajiliwa na Liverpool katika kipindi hiki cha usajili cha majira ya joto chini ya Kenny Daglish.

Tuesday, August 30, 2011

Sneijder: Siondoki Inter Nabaki

Wesley Sneijder

Wesley Sneijder, hatimae amemaliza kile kilichokuwa kinaaminika kinaweza kutokea katika kipindi hiki cha uhumisho kinachomalizika kesho huko barani Ulaya, na hii baada ya leo hii kutangaza rasmi nia yake ya kuendelea kuichezea timu yake ya Inter Milan.

Sniejder kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akihusishwa na kuhamia kwenye Ligi kuu ya Uingereza, huku timu za Chelsea, Manchester City na United zikiwa zinamfatilia kwa karibu.

Sneijder alieleza Sender Nos.  " Ninabaka hapa Inter, Sidhani kama nitaweza kuondoka katika kipindi hiki, Kuhusu Manchester United? Chochote kinaweza kutokea ila sidhani kama kuna lolote linaloweza kutokea kwa sasa.
"Najua kama ningepaswa kuondoka basi ingenibidi niondoke kwa bei muafaka, na hiyo ilikuwa wazi. Ila hakika sijawahi kuwa na mazungumzo rasmi na moja ya vilabu viwili vya Manchester.

Messi apewa Unahodha wa Argentina

Lionel Messi

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Argentina Alejandro Sabella, amemkabidhi rasmi unahodha wa timu ya taifa ya Argentina nyota wa timu ya Barcelorna Lionel Messi.

Tofauti na anayokuwa na timu yake ya Barcelona, Messi amekuwa na wakati mgumu wa kuonyesha makali yake akiwa na timu yake ya taifa, akishindwa kuisaidia timu yake kwenye mashindano ya kombe la Dunia ya mwaka 2010 na yale ya Copa America yaliyoisha hivi karibuni nchini mwao.

Sabella, ambaye alichukua mikoba ya ukocha toka kwa Sergio Batista kama Kocha wa Argentina mwezi huu, ameanza kufanya mabadiko kwenye timu hiyo kwa kumvika kitambaa cha unahodha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, kitambaa ambacho hapo awali kilikuwa kinavaliwa na mchezaji wanayecheza nae timu moja ya Barcelona  Javier Mascherano, Argentina wanavaana na Venezuela siku ya Ijumaa.

Poulsen awaita 30 Kikosi cha Ngorongoro Heroes

Kikosi cha Ngorongoro Heroes

KOCHA wa timu za vijana, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mazoezi mwezi ujao.

Poulsen alitangaza majina hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Aliwataja wachezaji hao na timu zao katika mabano kuwa ni Saleh Ally (TSA), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Mustapha (Polisi Dodoma), Andrew Kasembe (Moro United), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Ally Teru (Simba), Said Ruhava (Kagera Sugar) na Samuel Mkomola (Azam).

Wengine ni Frank Damayo (JKT Ruvu), Omega Seme (Yanga), Atupele Green (Yanga), Thomas Ulimwengu (ABC Sweden) na Jerome Lambele (Moro United).

Pia wapo Simon Msuvan (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Alex Joseph (Majimaji), Ibrahim Rajab (Azam), Renatus Patrick (Polisi Dodoma), Abdallah Kilala (AFC), Rajab Zahir (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba).

Wengine katika orodha hiyo ni Alfred Amede (Russia), Khelf Hassan (Kenya), Emily Mgeta (TSC Mwanza), Ramadhan Salum (Simba), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting).

Wachezaji Stars wanaocheza soka la kulipwa wawasili


Wachezaji  wa Stars wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wamewasili kwenye kambi kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Algeria utakaochezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa.

Wachezaji waliowasili ni pamoja na Mbwana Samatta anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, beki Idrissa Rajabu wa Sofapaka ya Kenya, Danny Mrwanda na Abdi Kassim wanaocheza soka la kulipwa nchini Vietnam katika klabu ya DT Long An, kiungo Henry Joseph wa Konsivinger ya Norway na Athumani Machupa wa Vasuland IF ya Sweden.

Wambura alisema kiungo wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa Canada katika klabu ya Vancouver Whitecaps, Nizar Khalfan anatarajiwa kuwasili leo usiku tayari kujiunga na kambi ya timu hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura alisema Kassim, Mrwanda na Samatta waliwasili juzi wakati Joseph, Rajabu na Machupa waliwasili jana. 

Liverpool wakataa ofa ya Chelsea kubadilishana na Raul Meireles

Timu ya Liverpool imetupilia mbali ofa ya Chelsea ya kumtaka mchezaji wao Raul Meireles, inaelezwa Chelsea walikuwa tayari kutoa Paundi Millioni 8 huku Yossi Benayoun akijumuishwa kwenye hesabu hiyo.

Meneja wa timu ya Chelsea Andre Villas-Boas alishawahi kufanya kazi na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 wakati walipokuwa pamoja na timu ya Porto, kabla ya mchezaji huyo kujiunga na Vijogo hao wa Anfield kwa ada ya Paundi Milioni 11 msimu uliopita.

Chelsea wameamua kutaka kumsajili Meireles baada ya kushindwa kwenye jaribio lao la kutaka kumsajili kiungo wa timu ya Tottenham Luka Modric.

Joe Cole njiani kujiunga na Lille kwa Mkopo

Mchezaji wa timu ya Liverpool Joe Cole yupo mbioni kujiunga na timu ya Lille ya nchini Ufaransa kwa mkopo wa msimu mzima.
Inaaminika Queens Park Rangers na Tottenham Hotspur nao wanamtolea macho mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.