Tuesday, August 30, 2011

Wachezaji Stars wanaocheza soka la kulipwa wawasili


Wachezaji  wa Stars wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wamewasili kwenye kambi kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Algeria utakaochezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa.

Wachezaji waliowasili ni pamoja na Mbwana Samatta anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, beki Idrissa Rajabu wa Sofapaka ya Kenya, Danny Mrwanda na Abdi Kassim wanaocheza soka la kulipwa nchini Vietnam katika klabu ya DT Long An, kiungo Henry Joseph wa Konsivinger ya Norway na Athumani Machupa wa Vasuland IF ya Sweden.

Wambura alisema kiungo wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa Canada katika klabu ya Vancouver Whitecaps, Nizar Khalfan anatarajiwa kuwasili leo usiku tayari kujiunga na kambi ya timu hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura alisema Kassim, Mrwanda na Samatta waliwasili juzi wakati Joseph, Rajabu na Machupa waliwasili jana. 

No comments:

Post a Comment