Wednesday, August 31, 2011

Chelsea yakaribia kumnasa Pereira

Alvaro Pereira

Wakala wa mchezaji Alvaro Pereira anayekipiga na timu ya Porto, amesema wako kwenye mazungumzo na timu ya Chelsea juu uwezekano wa kumsajili mchezaji wake.

Bosi wa timu ya Blues Andre Villas-Boas anamfahamu vyema mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay toka kipindi walichokuwa pamoja cha Estadio do Dragao wakiwa na timu ya Porto, na sasa anataka kuungana tena na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.

Mchezaji huyo aliyewahi kuchezea CFR Cluj na Argentinos Juniors, kwa sasa anasubiri kusikia kiasi cha fedha kitakachopitishwa ili aweze kukamilisha usajili wake, na wakala wake Alejandro Savich kwa sasa yupo nchini Uingereza akishughulikia suala hilo.

Timu kama Barcelona, AC Milan na Inter Milan nazo zimetajwa kumtaka mchezaji huyo.

Hii ni mara ya pili kwa Chelsea kutaka kumsajili mchezaji huyo, baada ya maombi yao ya mara ya kwanza kutolewa nje.

No comments:

Post a Comment