Monday, August 29, 2011

Arsenal kuwapa washabiki wake ofa ya tiketi za Bure

Club ya Arsenal imetangaza kuwapa ofa ya tiketi za bure washabiki wake waliohudhuria kwenye mechi ambayo iliisha kwa timu hiyo kufungwa na Man United kwa jumla ya magoli 8-2.

Imeelezwa inapata washabiki 3,000 walisafiri umbali wa Maili 400 kwenda kuona mchezo huo, ambao uliisha kwa kipigo cha aibu kwa timu yao.

Taarifa toka Club hiyo zimesema, mashabiki wa timu hiyo waliohudhulia mechi hiyo watapewa ofa hiyo kwenye moja kati ya mechi za ugenini itakayochezwa na timu hiyo.

No comments:

Post a Comment