Wednesday, August 31, 2011

Arsenal Yawasajili Mikel Arteta, Yossi Benayoun na Per Mertesacker


Mikel Arteta

Klabu ya Arsenal imemsajili beki wa Everton Mikel Arteta kwa kiasi cha £10m,  hii ni baada ya mchezaji huyo kutuma maombi ya kuhama.

Kiungo huyo wa ki-spania amejiunga na washika bunduki hao kwa mkataba wa miaka minne, na hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya dirisha la usajili kufungwa saa tano kamili kwa saa za Uingereza.

Arsenal pia imefanikiwa kumpata kwa mkopo mchezaji wa Chelsea Yossi Benayoun, kwa msimu mmoja.

Benayoun, ambaye ni nahodha wa nchi yake ya Israel, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema "Nimesajili na Arsenal, nina furaha sana na kupendezwa na jambo hili, ila kwa sasa kichwa changu kinafikiria juu ya mechi dhidi ya Ugiriki hapo Ijumaa, asanteni kwa ushirikiano wenu."

Klabu zote mbili zimethibitisha juu ya maafikiano hayo.

Pia imefahamika kwamba Arsenal wamekamilisha usajili wa Beki wa kimataifa wa Ujerumani Per Mertesacker toka Werder Bremen.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, inaaminika amewagarimu washika bunduki wa Emirates kiasi cha  £8m huku akiwa amesaini mkataba wa muda mrefu.

"Nilikuwa na wakati mzuri na Werder, hakika nawaheshimu sana, ila kuhamia London ni kama ndoto iliyokuwa kweli," alisema Mertesacker huku akiongeza "Kwangu mimi English Premier League mara zote naiona ina mvuto ikiwa na ushindani wa hali ya juu"

Meneja wa timu hiyo Arsene Wenger aliieleza kwenye mtandao wa timu hiyo: "Tumefurahi kumkaribisha Per Mertesacker kwenye Klabu yetu."

No comments:

Post a Comment