Msafara wa watu 50 wa timu ya soka ya taifa ya Algeria unawasili nchini leo tayari kwa
ajili ya mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 3.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kwamba Algeria itafika leo kwa ndege ya kukodi na baada ya kuwasili itaenda moja kwa moja katika hoteli ya Golden Tulip ambako watafikia.
Aidha, Wambura alisema kwamba waamuzi wote katika mchezo huo watatoka Mauritania huku kamisaa wa mchezo huo atakuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicolas Musonye.

No comments:
Post a Comment