Friday, August 26, 2011

Afrika Kusini mwenyeji wa KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2013 badala ya LIBYA


Afrika ya Kusini imesema wao ndio watakao kuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2013 badala ya Libya.

Nchi hizo mbili zimefikia makubaliano hayo huku zikibadilishana haki ya kuandaa mashindano hayo, hiyo ikimaanisha kwamba Libya itaandaa mashindano ya mwaka 2017 ambayo yalikuwa yandaliwe na Afrika ya... Kusini.

Dili hilo lilitangazwa na Chama Cha Soka cha Afrika ya Kusini (Safa), na suala hili sasa linasubiri ridhaa ya Chama Cha Soka Afrika (Caf).

Maandalizi ya Libya kuandaa michuano hiyo kwa mwaka 2013 yamekuwa kwenye mashaka kwa kipindi sasa, na hii ni kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo kwa sasa.
See More

No comments:

Post a Comment