Tuesday, August 30, 2011

Arsenal kukamilisha usajili wa Per Mertesacker

Kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Low amethibitisha kumpa ruhusa mchezaji wa timu hiyo Per Mertesacker kuondoka kwenye kambi ya timu hiyo ili aweze kwenda Lonon kukamilisha mpango wake Arsenal.

Mchezaji huyo beki wa timu ya Werder Bremen mwenye umri wa miaka 26 aitwae Mertesacker, anategemea kufanya vipimo na washika bunduki hao leo hii Jumanne, vipimo ambavyo kama akifaulu vitamuwezesha kujiunga moja kwa moja na timu hiyo inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment