Friday, August 26, 2011

Tottenham wakabidhiwa wabaya wao

Klabu ya soka ya Tottenham ya Uingereza ambayo msimu uliopita ilishiriki Ligi ya mabingwa wa Ulaya na kuchachafya baadhi ya vigogo kabla ya kutolewa na Real Madrid, itajaribu tena bahati yake katika michuano ya Ulaya msimu huu kwa kuumana na Rubin Kazan, PAOK Salonika, pamoja na Shamrock Rovers.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jioni ya leo na shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya (UEFA), kwa michuano ya ligi ya washindi barani humo, Spurs wako kundi A, sanjari na timu hizo, na wadadisi wa masuala ya soka wameonyesha wasiwasi wao kwa kulielezea kundi hilo kuwa si rahisi kama ambavyo linaweza kuonekana machoni mwa watu kwa kusoma.
Katika ratiba hiyo, timu nyingine za Uingereza za Stoke City, Fulham, pamoja na Birmingham, nazo zimepangwa katika makundi tofauti tofauti, huku pia makundi yao yakielezwa kuwa si mchekea.
Makundi hayo kwa mujibu wa UEFA ni kama ifuatavyo:
Group A: TOTTENHAM, Rubin Kazan, PAOK Salonika, SHAMROCK ROVERS
Group B: FC Copenhagen, Standard Liege, Hannover, Vorskla Poltava
Group C: PSV Eindhoven, Hapoel Tel-Aviv, Rapid Bucharest, Legia Warsaw
Group D: Sporting Lisbon, Lazio, FC Zurich, FC Vaslui
Group E: Dynamo Kiev, Besiktas, STOKE, Maccabi Tel-Aviv
Group F: Paris St Germain, Athletic Bilbao, Salzburg, Slovan Bratislava
Group G: AZ Alkmaar, Metalist Kharkiv, Austria Vienna, Malmo
Group H: Braga, Club Brugge, BIRMINGHAM, Maribor
Group I: Atletico Madrid, Udinese, Rennes, Sion
Group J: Schalke, Steaua Bucharest, Maccabi Haifa, AEK Larnaca
Group K: FC Twente, FULHAM, Odense, Wisla Krakow
Group L: Anderlecht, AEK Athens, Lokomotiv Moscow, Sturm Graz

No comments:

Post a Comment