Wednesday, August 31, 2011

Raul Meireles wa Liverpool ahamia Chelsea

Raul Meireles

Kiungo wa Liverpool Raul Meireles, amefanya uhamisho wa aina yake na kujiunga Chelsea kwa thamani ya £12m.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alituma maombi ya kuhama Anfield muda mfupi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, na ameweza kuingia mkataba wa miaka minne na watoto wa darajani.

Meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas aliwahi kufanya kazi sambamba na mchezaji huyo walipokuwa Porto kabla ya mchezaji huyo kuelekea Anfield mnamo mwezi August mwaka jana.

Meireles kwa sasa ni majeruhi, baada ya kuumia kwenye mechi ya Liverpool ilipocheza na Exeter City kwenye kombe la Carling mapema wiki iliyopita.

Mwanzoni Liverpool waliikataa ofa ya Chelsea kwa mchezaji huyo, ambapo walikuwa wapo tayari kutoa £8m sambamba na Yossi Benayoun ili kuweza kumpata.

No comments:

Post a Comment