Monday, August 29, 2011

Gurumo jukwaa Idd Mosi

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Muhidin Gurumo anatarajiwa kupanda jukwaani Idd Mosi mwaka huu akiwa na bendi yake ya Msondo Ngoma Music.

Gurumo hajaonekana jukwaani kwa muda mrefu sasa kutokana na kuwa mgonjwa, lakini Msondo imepanga bonanza maalumu litakalofanyika viwanja wa Sigara, Chang’ombe Dar es Salaam siku ya Idd el Fitri.

No comments:

Post a Comment