Tuesday, August 30, 2011

Arsenal wakamilisha usajili wa Park Chu-Young

Klabu ya Arsena imethibitisha kwamba wamekubaliana na timu ya Monaco juu ya uhamisho wa mchezaji wa timu hiyo Chu Young Park.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 raia wa Korea ambaye pia ni Captain wa nchi hiyo, ameifungia timu ya Monaco jumla magoli 25 kwenye mechi 91 alizoichezea kwa misimu mitatu kwenye ligi ya nchi hiyo maarufu kama Ligue 1.
 
Mchezaji huyo amewahi kushinda tuzo ya mwanasoka chipukizi wa mwaka wa bara la Asia, alianza kuichezea timu ya taifa ya Korea akiwa na umri wa miaka 19, aliichezea timu yake ya taifa kwenye mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2006 na 2010. Kwa sasa mchezaji huyo ndiye Captain wa nchi yake na hii ni baada ya kuchukua nafasi ya captain aliyestaafu Ji Sung Park mapema mwaka huu.

No comments:

Post a Comment