Friday, August 26, 2011

Man City wakamilisha usajili wa Nasri

Club ya manchester City imekamilisha rasmi usajili wa aliyekuwa kiungo wa Arsenal Samir Nasri, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka 4 pale Etihad, vyanzo vya karibu vimesema dau lililotumika kumnasa kiungo huyo linakadiliwa kuwa kiasi cha paundi Millioni 24.

Pia imeelezwa kwamba mchezaji huyo wa kifaransa anategemea kuwemo kwenye mechi ya jumapili ambapo Man city watacheza na timu ya Tottenham kwenye uwanja wa White Hart Lane, na atakuwa anavaa jezi namba 19.

No comments:

Post a Comment