Monday, August 29, 2011

Arsenal, Liverpool na Lille wamsaka Yossi Benayoun

Arsenal, Liverpool na timu ya Ufaransa Lille, wameonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Chelsea Yossi Benayoun.

Mchezaji  huyo raia wa Israel mwenye umri wa miaka 31hivi karibuni kupitia mtandao Twitter alieleza nia yake ya kuondoka kwenye timu hiyo ya Stamford Bridge.

Arsenal wanaonekana wako nia ya dhati kumchukua mchezaji huyo, ili wawaeze kuziba mapengo yaliyoachwa na wachezaji wake Cesc Fabregas na Samir Nasri.

Benayoun alijiunga na Chelsea toka Liverpool kwa thamani ya £5m, mnamo mwezi July 2010 huku akibahatika kupata nafasi ya ya kucheza kwa dakika moja tu toka msimu mpya uanze.

No comments:

Post a Comment